Friday, January 15, 2010

IJUMAA WIKIENDA!

Besta

Nameless

Mr. Lenny

Nonini

Juacali

East Afrika nani mkali? Wa Bongo ni aibu stejini....

Wiki iliyopita tuliwaletea wakali kutoka kiwanja waliopiga shoo ya kiwango cha juu Bongo. Tulimtaja Akon nambari one, pili P-Square, tatu Busta Rhymes, Fat Joe akadaka nafasi ya nne na 50 Cent alikuwa wa tano.

Hata hivyo, leo ni zamu yako kutueleza ni nani mkali wa kupiga shoo Afrika Mashariki kulingana na jinsi ulivyowaona artists mbalimbali utoka Kenya na Uganda waliowahi kudondoka Bongo.

Bila shaka unamjua mkali, kwahiyo piga kura yako kwa njia ya SMS kwenda
namba 0715-110 173, kisha utajisoma hapa wiki ijayo.

Artists wa Bongo ni aibu jukwaani!
Wakali wa muziki wa kizazi kipya wanaua bendi. Inaonekana baadhi yao ndiyo chanzo cha kuporomoka kwa soko la Bongo Flava. A problem ni kwamba wakiwa jukwaani hawajui kusisimua, wamezorota ile mbaya.

Hawajifunzi, wakali wanaotoka nje wakitua Bongo wanafanya wonders jukwaani kwa kutoa shoo ya nguvu, lakini wao kila siku ni pale pale. Hawasisimui, kelele nyingi, lakini anabaki amesimama sehemu moja utafikiri kapigiliwa misumari.

Ni wachache ambao wanaweza kazi, angalau siku hizi Alikiba a.k.a Ali Saleh Kiba, A.Y, Nako 2 Nako na wengineo wachache, wakiwa jukwaani huonesha madoido fulani fulani lakini wengine wengi ni matatizo.

Kama ni Hip Hop, swagger hakuna, wanaoimba wanabaki kuwa wazuri wa kupiga kelele, hata kujitikisa wanashindwa. Ukiwaambia waajiri wachezaji, wanakwambia muziki haulipi.

Utaona wakali kutoka Kenya kama Juacali, Nonini, Nameless na wengineo, wakiwa jukwaani utakubali kwamba mwanamuziki yupo kazini. Kule Uganda watu kama Bobby Wine, Chameleon, Bebe Cool na wengineo, wanajua nini maana ya kulitumia jukwaa. Hili linawafanya wao waonekane bora, sisi tunaonekana tupo tupo. Ni aibu!

Ni uvivu wa kufikiria shoo na kujituma katika kuandaa burudani yenye kiwango. Mastaa wetu ni wazuri kwa kusikiliza tungo zao redioni au kwenye televisheni lakini si kuwashuhudia jukwaani. Badilikeni nanyi mvutie.
****************************************

Missy Elliot anyanyuka na Lil Wayne
Mwana Hip Hop mwenye skandali la usagaji, La Shawn Shellman ‘Missy Damina Elliot’ ameamua kuvunja ukimya na hivi sasa kwa kutumia lebo yake ya Background, ananyanyuka kitaani na singo kali inayokwenda kwa jina la All 4 U ambayo amempa featuring, Lil Wayne.

Stori kwamba Missy Eliot is back to her position, zimepenyezwa na mtandao wa Twitter ambao umemnukuu mgumu huyo wa kike kwamba anarudi vizuri baada ya kukaa kimya muda mrefu akitafakari game inakwendaje.



T.I. auanza mzigo kwa fujo
Few days baada ya kuwa released lupango, staa wa The Live Your Life, Clifford Harris Jr. a.k.a T.I ameaunza mzigo kwa fujo na kwa sasa yupo tayari kuachia albamu yake mpya ambayo mpaka sasa hajaamua jina la kuipa.

Very direct from Atlanta, Georgia ambako T.I anafanya life yake, mchizi huyo alisema kuwa anataka kuwapa mashabiki wake hali halisi ya maisha yake alipokuwa nyuma ya nondo na kuongeza kuwa alisubiri 2010 itimie na sasa ipo tayari.



Daz Nundaz ni huzuni nyingine
its another sad story about lile kundi lililowahi kuitikisa Bongo mwanzoni mwa miaka ya 2000, Daz Nundaz kuwa hata nini kifanyike, ni ngumu kulirudisha kwasababu wasanii wenyewe hawajaamua kutulia na kushirikiana kufanya kazi.

Mpya tuliyoipata this week ni kuwa jitihada za mwanzo za kuwarudisha Daz kwenye position yao the time walipo hit na Maji ya Shingo, Barua na Kamanda zimegonga ukuta baada ya kichwa namba moja wa kundi, Ferouz Mrisho kuamua kuwatosa wenzake.

Showbiz imebaini kuwa baada ya shoo ya Fiesta 2009 (One Love)ambapo Daz Nundaz walipanda jukwaani pamoja, kulikuwa na promise ya kufanya kazi together as one, lakini baada ya siku chache Ferouz aliwaambia wenzake kwamba hayupo tayari kushirikiana.

“Baada ya Ferouz kujitoa, Daz Baba (David Nyika) naye akasema atafanya kazi kivyake, kwahiyo kundi limekufa, halipo,” alisema mmoja wa memba wa Daz.


1 comment:

Anonymous said...

habari ndugu mimi ni mmoja wa wasomaji wa magazeti yenu yote yaliyochini ya global publishers ni chanzo changu kikubwa cha habari za huko nyumbani kwani ninaishi nje ya nchi sa haya mabadilko yananipa tabu kidogo nikiclick kujiregister hauvunguki ukurasa hou sasa tatizo ni pc yangu awu kwa wote asante.issaisteven@gmail.com