Monday, January 11, 2010

Ni kweli featuring zinaua biashara?

Mh. Temba

Pharel Williams
Chid benz
Imekuwa ni wimbo sasa, artists wa Bongo wanaigana kutoa matamko. Kauli ya mchizi fulani kachaa huyu naye anairudia. Hatuoni mwenye mtazamo wake binafsi, pia inaonekana hawaumizi vichwa inavyotakiwa.

Gumzo hapa ni featuring, mastaa wa Kibongo hawataki kushirikishwa kwenye nyimbo za wenzao hasa underground kwa sababu eti wanapoingiza vocal kwenye mawe ya wengine, wakitoa yao yatadoda.

Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, Abdul Sykes ‘Dully’, Aboubakar Katwila ‘Q Chillah’ na wengineo, kwa nyakati tofauti wamejikuta ni waumini wa kauli hiyo. Wanasema kukamua kwenye nyimbo za wengine, kunaharibu soko la muziki wao, kwahiyo wanaona ili kutetea hilo ni bora wapunguze.

Wana hoja ya msingi? Ni vema kuheshimu mtazamo wao lakini ukweli ni kwamba wanachokiongea ni uoga! Na pengine hawana data ndiyo maana wanathubutu kutamka maneno hayo.

Ukweli ni huu, featuring haiui soko la mtu bali linakuza. Mtu anayeshirikishwa kwenye nyimbo za wengine na anafanya vizuri, uchunguzi unaonesha kuwa huwa anakubalika mno kijamii, hivyo kwake ni rahisi kuuza kuliko yule anayenyuti kungoja jiwe lake liingie sokoni.

Hii inamaana kuwa msanii anayevunja vilivyo kwenye pini za watu, maana yake anajenga imani kwa mashabiki kwamba uwezo wake ni mkubwa, wanakuwa wanatamani kumsikia katika kazi yake mwenyewe, na akidondosha goma lazima litolewe macho na kama lipo bomba hapo kinachofuata ni full mauzo.

Ikitokea unafanya vizuri kwenye nyimbo za watu halafu ya kwako ukiharibu, hiyo ni ishu nyingine. Na katika hilo usithubutu kusema eti featuring ndiyo zinazokutoa knock out, ubovu wa muziki wako ndiyo chanzo.

Mifano; Pharel William alikuwa juu wakati anagonga featuring kwenye ngoma za wenzake, na alipofanya mradi wa The Neptune’s alipiga bao ile mbaya, leo kimya cuz hagongi vocal kwenye singo za wenzake hata income imepungua na hata akitaka kutoka itabidi afanye promo ya nguvu.

Hapa Bongo, kumbuka enzi zile Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’, Haroun Kahena ‘Inspector, Babu’, Dully, Q Chillah, Ferouz Mrisho na wengine wapo kileleni, walikuwa wanafanya featuring nyingi na biashara yao ikawa inakwenda byee byee!

Tuseme ukweli, wote hao sasa hivi siyo kama zamani na hawafanyi featuring. So, ukweli unabaki pale pale, kushirikishwa kwenye nyimbo nyingi na ukifanya vizuri ni poa sana kibiashara kwa sababu siku ukitaka kutoka mwenyewe, haikulazimu upate promo ya nguvu cuz watu wanakujua na kazi zako zinakubalika.
*******************

No comments: