Mkono Mmoja Yawakutanisha Wahu, Michael Ross Bongo
Usiku wa Mkono mmoja ambao ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Club Sun Ciro huku vichwa kutoka TMK Wanaume, Chegge na Temba vikitambulisha albamu yao, Vita uwanjani, uliwakutanisha pia mastaa wawili kutoka Afrika Mashariki, Wahu wa Kenya na Michael Ross kutoka Uganda.
Shoo hiyo ambayo ilianza majira ya saa sita za usiku ilimpa shavu la ukweli Michael Ross ambaye alipanda stejini kupitia juu ya paa la ukumbi huo kabla hajashuka chini na kuanza kuonesha uwezo wake jukwaani huku akiamsha shangwe kutoka kwa mashabiki waliofurika siku hiyo.
Aliyefuatia alikuwa ni Wahu ambaye pia aliufanya usiku huo kuwa wa burudani kabla vijana wa TMk kupanda na kumaliza kazi kwa staili mpya kabisa iliyotawaliwa na shoo ya kiduku kabla hawajamaliza kwa ngoma ya Mkono mmoja iliyomshirikisha Wahu. Msanii Goodzila alitoa sapoti ya nguvu huku shoo nzima ikisimamiwa na B-12 wa kipindi cha XXL cha Clouds FM.
Kama walivyoahidi wasanii wa kundi la muziki wa asili kutoka Botswana, Makhirikhiri walipodondoka ndani ya ofisi za gazeti hili katikati ya wiki iliyopita, ndivyo walivyofanya juzi ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambapo waliangusha shoo ya kihistoria.
Wakiongozwa na Shumba Ratshega, Makhirikhiri waligonga staili zao zote ambazo zimetokea kuwavutia mashabiki wengi wa muziki wao tangu walipoanza kulifahamu kundi hilo lililojipatia umaarufu wa ghafla Bongo na kusababisha shangwe zilipuke kwa sana ukumbini.
Baada ya kufanya maajabu Diamond, jamaa walihamishia majeshi ndani ya Uwanja wa Uhuru jana Jumapili na kuacha historia kwa wakazi wa Dar. Makhirikhiri ambao wanaendelea na ziara yao Mkoani Mbeya walipigwa tafu na Wanne Star na mwanadada Mwantum Chambali kutoka kundi la Mshikamano ambaye anatisha kwenye mchezo wa kujinyonganyonga maarufu kama Yoga.
Kutoka pande za mbele a.k.a Marekani leo ndani ya Ebwana Dah! tunacheki listi ya uhusiano wa kimapenzi ya mmoja kati ya waasisi wa muziki wa Hip Hop, Russell Simmons ambaye hivi sasa ameamua kujikita zaidi kwenye biashara ya mavazi, huku akimiliki logo kadhaa ikiwemo ‘Phat Farm’. Ni maombi ya wasomaji wengi wa safu hii hapa Bongo, hasa baada ya kuenea kwa picha za tajiri huyo na mwanamitindo wetu, Flaviana Matata kwenye mtandao.
Kama bado haujafahamu, Russell amewahi kujiachia on bed na mastaa wa kike tisa kabla ya kudondokea kwa Noemie Lenoir (picha kubwa) mwaka jana wa 2010. Lakini pamoja na hao mchizi kutoka ndani ya kundi la Out Cast, ‘brazameni’ Andre Benjamin pia ametajwa kwenye listi ya watu waliowahi kujiachia faragha na Russell kitu ambacho kinaweza kumshangaza kila msomaji ukizingatia kwamba hawa jamaa wote ni wanaume.
Tukirudi kunako listi ya warembo hao, Russell alianza kutoka na Eva Pigford ambaye nyota yake ni Nge akifuatiwa na Karin Taylor, kisha Karrine Steffans, Veronica Webb, Kara Young (1994 - 98), Kimora Lee Simmons ambaye ndiye alikuwa mkewe baada ya kufunga ndoa 1998 kabla ya kupigana chini 2006, kisha kurudiana tena na kuachana moja kwa moja 2009.
Kabla hajaachana na Kimora, Russell alicheza game ya nje ya ndoa kwa kujiachia na mwanadada Porschla Coleman kuanzia 2007 - 08. Baada ya kuachana na Kimora mchizi alitua kwa Julie Henderson 2009 kisha Noemie Lenoir 2009.
Russell alizaliwa pande za Queens, New York, Oktoba 4, 1957, jina lake kamili ni Russell Wendel Simmons. Akiwa na umri wa miaka 52 sasa na urefu wa nchi 5 na futi 8, mchizi alihitimu elimu ya juu katika vyuo vya City College of New York na Harlem vilivyopo huko New York.
Usiku wa Mkono mmoja ambao ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Club Sun Ciro huku vichwa kutoka TMK Wanaume, Chegge na Temba vikitambulisha albamu yao, Vita uwanjani, uliwakutanisha pia mastaa wawili kutoka Afrika Mashariki, Wahu wa Kenya na Michael Ross kutoka Uganda.
Shoo hiyo ambayo ilianza majira ya saa sita za usiku ilimpa shavu la ukweli Michael Ross ambaye alipanda stejini kupitia juu ya paa la ukumbi huo kabla hajashuka chini na kuanza kuonesha uwezo wake jukwaani huku akiamsha shangwe kutoka kwa mashabiki waliofurika siku hiyo.
Aliyefuatia alikuwa ni Wahu ambaye pia aliufanya usiku huo kuwa wa burudani kabla vijana wa TMk kupanda na kumaliza kazi kwa staili mpya kabisa iliyotawaliwa na shoo ya kiduku kabla hawajamaliza kwa ngoma ya Mkono mmoja iliyomshirikisha Wahu. Msanii Goodzila alitoa sapoti ya nguvu huku shoo nzima ikisimamiwa na B-12 wa kipindi cha XXL cha Clouds FM.
****************************************
Makhirikhiri Wamaliza kazi kwa kufunika Dar Kama walivyoahidi wasanii wa kundi la muziki wa asili kutoka Botswana, Makhirikhiri walipodondoka ndani ya ofisi za gazeti hili katikati ya wiki iliyopita, ndivyo walivyofanya juzi ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambapo waliangusha shoo ya kihistoria.
Wakiongozwa na Shumba Ratshega, Makhirikhiri waligonga staili zao zote ambazo zimetokea kuwavutia mashabiki wengi wa muziki wao tangu walipoanza kulifahamu kundi hilo lililojipatia umaarufu wa ghafla Bongo na kusababisha shangwe zilipuke kwa sana ukumbini.
Baada ya kufanya maajabu Diamond, jamaa walihamishia majeshi ndani ya Uwanja wa Uhuru jana Jumapili na kuacha historia kwa wakazi wa Dar. Makhirikhiri ambao wanaendelea na ziara yao Mkoani Mbeya walipigwa tafu na Wanne Star na mwanadada Mwantum Chambali kutoka kundi la Mshikamano ambaye anatisha kwenye mchezo wa kujinyonganyonga maarufu kama Yoga.
************************************
Russel Simmons Hiki ndiyo kifaa chake, baada ya kuwapitia wengine 9Kutoka pande za mbele a.k.a Marekani leo ndani ya Ebwana Dah! tunacheki listi ya uhusiano wa kimapenzi ya mmoja kati ya waasisi wa muziki wa Hip Hop, Russell Simmons ambaye hivi sasa ameamua kujikita zaidi kwenye biashara ya mavazi, huku akimiliki logo kadhaa ikiwemo ‘Phat Farm’. Ni maombi ya wasomaji wengi wa safu hii hapa Bongo, hasa baada ya kuenea kwa picha za tajiri huyo na mwanamitindo wetu, Flaviana Matata kwenye mtandao.
Kama bado haujafahamu, Russell amewahi kujiachia on bed na mastaa wa kike tisa kabla ya kudondokea kwa Noemie Lenoir (picha kubwa) mwaka jana wa 2010. Lakini pamoja na hao mchizi kutoka ndani ya kundi la Out Cast, ‘brazameni’ Andre Benjamin pia ametajwa kwenye listi ya watu waliowahi kujiachia faragha na Russell kitu ambacho kinaweza kumshangaza kila msomaji ukizingatia kwamba hawa jamaa wote ni wanaume.
Tukirudi kunako listi ya warembo hao, Russell alianza kutoka na Eva Pigford ambaye nyota yake ni Nge akifuatiwa na Karin Taylor, kisha Karrine Steffans, Veronica Webb, Kara Young (1994 - 98), Kimora Lee Simmons ambaye ndiye alikuwa mkewe baada ya kufunga ndoa 1998 kabla ya kupigana chini 2006, kisha kurudiana tena na kuachana moja kwa moja 2009.
Kabla hajaachana na Kimora, Russell alicheza game ya nje ya ndoa kwa kujiachia na mwanadada Porschla Coleman kuanzia 2007 - 08. Baada ya kuachana na Kimora mchizi alitua kwa Julie Henderson 2009 kisha Noemie Lenoir 2009.
Russell alizaliwa pande za Queens, New York, Oktoba 4, 1957, jina lake kamili ni Russell Wendel Simmons. Akiwa na umri wa miaka 52 sasa na urefu wa nchi 5 na futi 8, mchizi alihitimu elimu ya juu katika vyuo vya City College of New York na Harlem vilivyopo huko New York.
Compiled by mc george/ijumaa wikienda
No comments:
Post a Comment