Friday, August 20, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

Lloyd Banks Aipaisha Bongo
Mkali wa Muziki wa Hip Hop kutoka kruu ya G-Unit inayowakilisha kutoka pande za New York, Marekani, Lloyd Banks amelipa fadhila za shangwe alizopewa na mashabiki alipokuja kufanya shoo Bongo akiwa na 50 Cent mwaka 2008, baada ya kushusha ngoma mpya ambayo ndani yake ina mashairi yanayozungumzia Bongo.

Ngoma hiyo inayokwenda kwa jina la Any Girl, aliyomshirikisha staa kutoka lebo ya Murder Inc aitwaye Lloyd Polite Jr, imelipa shavu la kutosha Bongo.
““Nimefanya shoo nyingi Ulaya na Amerika lakini kwa Afrika siku zote nimekuwa siisahau Tanzania ndiyo maana nimeamua kuzungumza kitu kuhusu nchini hii, kwangu mim ni nchi nzuri na nimeipenda sana,” alisema katika mtandao mmoja wa burudani nchini Marekani.

Baadhi ya mistari inayosikika katika mashairi ya pini hilo ni kama hivi; ‘ Baby, I’m a millionair, got a show hoppin outta’ the leer in Tanzania.’

Promota: Sikumuomba penzi Ray C ila...
Baada ya kutupiwa lawama za kumtaka kimapenzi nyota wa muziki kutoka Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, promota maarufu wa muziki pande za ‘Nai’ (Nairobi) anayejulikana kwa jina moja la Saadat, ameibuka na kutupilia mbali madai hayo kuwa hakuwahi kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa habari kutoka mtandao wa kenyaonline, promota huyo alitanabaisha kuwa ingekuwa ni vigumu kwake kumualika nyota huyo wa Kitanzania kupiga shoo mara nyingi kama angekuwa amemtaka kimapezi pindi alipokutana naye hapa Bongo.

“Kama nilimtaka kimapenzi na akanichomolea kwanini nimemleta Kenya baada ya mwezi mmoja na nusu tangu nikutane naye Tanzania? Je, kama nilikuwa namtaka ningewalipia tiketi ya ndege yeye na boyfriend wake Lord ili waje Kenya? Je, hivyo ndivyo angefanya mtu ambaye anamtaka mwanamke kimapenzi?” Alihoji promota huyo na kukaririwa na mtandao huo unaojihusisha na mambo ya mastaa nchini humo.

Nasaka mahela kwenye filamu na muziki- H . BABA
Siku chache kabla ya kudondosha sinema yake mpya kitaani iliyopewa jina la Promota, mkali wa miondoko ya TAKEU Bongo, Hamis Ramadhani a.k.a H. Baba amekanusha stori pepe zilizozagaa mtaani kuwa ameuweka kando muziki.

Akizungumza na ShowBiz hivi karibuni jijini Dar, mkali huyo mwenye vipaji lukuki aliweka kweupe kuwa, ishu ya yeye kugonga muvi isitafsiriwe kama katoa mkono wa kwaheri kwenye muziki kwani anasaka mahela kote kote.

Huyu hapa anafafanua: “Siyo kweli kuwa nimeacha muziki, mimi ni msanii hivyo nina nafasi ya kufanya aina yoyote ya sanaa hapa duniani, iwe muziki, filamu, maigizo, sarakasi na mazingaombwe, hizo zote ni kazi zangu na ndiyo maisha yangu, siwezi kuacha muziki hata siku moja.” Mzigo huu umeshushwa na Hemed Kisanda.

Chipukizi wa filamu wamtolea chozi JB
Baadhi ya wasanii chipukizi wa filamu Bongo wamemtolea chozi staa anayetesa kwenye field hiyo, Jacob Steven ‘JB’ wakimtaka awashirikishe kwenye sinema zake ili watoke kisanii, muziki mzima unaletwa na Jelard Lucas.

Akizoza na kona hii juzi Jumatano, jijini Dar es Salaam, alipokutana uso kwa macho na paparazi wetu, JB alisema mara kwa mara amekuwa akiombwa na wasanii chipukizi awashirikishe kwenye filamu zake.

“Labda niweke wazi kwamba, sasa nataka kuwasaidia kwa dhati kabisa, kama wewe ni chipukizi na unajua una kipaji, tuwasiliane,” alisema JB na kuongeza: “Unajua leo tupo, kesho hatupo kwahiyo lazima tufungue milango ya kuwasaidia wale wenye vipaji ili tukiwa hatupo waweze kuchukua nafasi zetu. Mimi nimeamua kwa dhati kabisa, kuwasaidia kupitia Kampuni yangu ya Jerusalem Film Compony.”

ShowBiz inampa tano JB kwa uamuzi wake huo ambao kiukweli utainua vipaji vya wasanii wetu. Poa sana mwana!!!

2 comments:

emu-three said...

Hayo ni mambo ya mastaa, sasa uamini lipi?

Maisara Wastara said...

Kaazi kweli kweli