Monday, August 9, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!


Miaka 10 ya Binti Machozi: Gardner ‘full’ miluzi ukumbini, Keisha apaliwa na keki
Sherehe za kutimiza miaka 10 ya Bendi ya Machozi zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Kijitonyama jijini Dar zilitawaliwa na vijimambo vingi kimojawapo kikiwa ni kitendo cha Mtangazaji mahiri wa Clouds FM, Gardner G. Habash kutumia muda mwingi kupiga miluzi.

Safu hii ilimshuhudia mshkaji huyo ambaye ni mume wa Lady Jaydee akifanya hivyo kuonesha furaha aliyokuwa nayo huku mkononi akiwa ameshikilia kinywaji ambacho kilitajwa kuwa ni pombe.

Aidha, Gardner alionesha kuwa na utulivu ‘ziro’ kutokana na kitendo cha mara kwa mara kupanda jukwaani na kwenda kumsemesha mkewe wakati akiimba hali iliyowafanya baadhi ya mashabiki kuona anawaboa.

Wakati huo huo, Sitaduu anayepiga mzigo na Kundi la muziki la Tip T op Connection lenye maskani yake Manzese jijini Dar, Khadija Shabani ‘Keisha’, naye alijikuta akipaliwa na keki iliyoandaliwa na msanii mwenzake Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ kwa ajili sherehe hiyo.

Ishu ilikuwa hivi; wakati Jide akiwalisha mashabiki wake vipande vya keki, ilifika zamu ya Keisha ambapo alipoiweka mdomoni ilimpalia hali iliyomfanya apige kelele kumuita Gardner amuokoe.

Hata hivyo, zoezi la kumpatia huduma ya kwanza lilifanyika fasta ambapo mbunifu maarufu wa mavazi Bongo, Khadija Mwanamboka alichukua jukumu hilo ikiwa ni pamoja na kumpatia maji ya kunywa na baada ya muda mfupi alirejea katika hali yake ya kawaida .

Licha ya matukio hayo, sherehe hizo zilifana vilivyo huku maelfu ya mashabiki wakijitokeza kumuunga mkono msanii huyo.
************************************************
Dida atangaza uchumba na mlemavu
‘Prezenta’ wa Kipindi cha Mirindimo ya Pwani kinachorushwa hewani kupitia Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ juzi kati alionesha kushobokea penzi la mshkaji mmoja mlemavu ambaye jina lake hatujalinyaka mara moja baada ya kutangaza uchumba naye.

Tukio hilo lilichukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Gaddafi Square uliopo Buza ndani ya Jiji la Lukuvi ambapo Dida alikuwa MC katika shoo maalum ya Kundi la Taarab la Super Shine.

Awali, mlemavu huyo alipanda jukwaani na kuomba kupiga picha na Dida, baada ya zoezi hilo mtangazaji huyo alimkumbatia na kuutangazia umma kuwa, huyo ndiye alikuwa mchumba wake na kwamba asijitokeze mwanamke yeyote akamshobokea.

Baada ya kutoa kauli hiyo, mashabiki waliokuwepo ukumbini hapo walishangilia lakini baadhi walibaki na vingi viulizo hasa kutokana na namna Dida alivyoendelea kumganda mlemavu huyo ndani ya ukumbi huo.

No comments: