Nami namlilia Leticia,
Poleni sana ndugu na wanahabari wote kwa msiba wa Leticia Kaijage. Namkumbuka sana dada Leticia wakati akitumikia gazeti la B/Times na baadaye pale The African mwaka 1998. Wakati ule tulikuwa na Florian Kaijage sasa yupo TFF na waandishi wengine mahiri wakiwemo akina Morice Maunya, Ongeri John, Alfred Mbogora, Amabilis Batamula, Nicodemus Odhiambo, Gerald Ndalawa na wengine wengi. Leticia pamoja na hao niliowataja walitusaidia sana katika kujifunza uandishi wa habari. Lakini Leticia ameendelea kuwa rafiki wa familia na waandishi wa habari hata baada ya kuondoka katika vyombo vya habari na kuwa Meneja/Ofisa Uhusiano katika kampuni mbalimbali. Daima tutamkumbuka Leticia Kaijage. Poleni sana wafiwa, poleni sana wanahabari. Bwana alitoa na Bwana ametwaa.....jina lake lihimidiwe. Neville C. Meena, Secretary General, Tanzania Editors' Forum (TEF), Dar es Salaam -Tanzania.
PICHA ZAIDI BONYEZA HAPA
PICHA ZAIDI BONYEZA HAPA
No comments:
Post a Comment