Siku zote ni muhimu sana kuwa na elimu ya kutosha katika kila jambo unalolifanya. Kufanya jambo usilokuwanalo elimu au ufahamu nalo ni sawa na mtu kutembea kwenye giza nene. Halikadhalika ni jukumu letu kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu vyakula tunavyokula.
Ukitaka kuzima moto, ni lazima ujue moto huo ni wa aina gani, kwa sababu siyo kila moto unazimwa kwa maji. Linapokuja suala la kutibu magonjwa, hatuna budi pia kujua dawa sahihi ya kutibu na pia kujua sababu zinochangia kupata ugonjwa huo.
UGONJWA WA SARATANI
Katika kukabiliana na ugonjwa huu hatari unaowakumba watu wengi duniani, watafiti wa tiba wa ugonjwa huu wamegundua orodha ya vyakula ambavyo huimarisha seli za saratani pale vinapoliwa na mtu ambaye tayari ameathirika na ugonjwa huo.
Kwa mantiki hiyo, ni jambo muhimu na la lazima sana kwa mgonjwa wa saratani (ya aina yoyote) kujua vyakula vinavyoimarisha ugonjwa wake badala ya kumpa nafuu, hivyo kulifanya tatizo kuwa sugu. Mgonjwa wa saratani anashauriwa kutovila kabisa vyakula vifuatavyo, kwa sababu ndiyo ‘chakula cha seli za saratani:’
SUKARI
Sukari tunayotumia kwenye chai na vyakula vingine ni ‘chakula kwa saratani’. Unapoacha kutumia kabisa sukari, unazikosesha chakula muhimu sana seli za ugonjwa huo na hivyo kudhoofika. Acha ulaji wa sukari na vyakula vyenye sukari, badala yake tumia asali au mbadala mwingine.
MAZIWA
Unywaji wa maziwa hutengeneza ‘ujiuji’ (mucus) kwenye utumbo ambao ni chakula cha seli za saratani, kwa kuacha unywaji wa maziwa utakuwa unadhoofisha chembechembe za saratani.
NYAMA
Chembechebe za saratani hustawi zinapoishi kwenye mazingira yenye asidi (acidic environment), lishe yenye nyama huwa na kiwango kikubwa ch asidi ambacho hustawisha saratani. Hivyo, badala yake mgonjwa anashauriwa kupenda kula samaki na kuacha nyama za ng’ombe, mbuzi, n.k.
KAHAWA
Mgonjwa wa saratania ana shauriwa kuacha kunywa kahawa, chai (majani meusi) na chokoleti ambazo zina kiwango kikubwa cha ‘alikalaini’ ambacho hustawisha saratani. Chai ya kijani (green tea) inaelezwa kuwa na virutubisho venye uwezo wa kupambana na chembechembe hai za saratani, yenyewe haina matatizo.
Mbali ya chakula, hali ya mtu nayo huweza kuchangia kuimarika kwa seli za saratani. Mtu mwenye ugonjwa huu hapaswi kuwa na hasira au wasiwasi kila mara, hali ambayo huzaliwa asidi mwilini, na tumeishaona hapo juu kuwa ugonjwa huimarika kwenye mazingira yenye asidi.
Mazoezi nayo ni muhimu kwa mgonjwa, ambayo yatamsadia kuongeza hewa ya oksijeni mwilini. Tumeona kuwa chembechembe za saratani haziwezi kuimarika kwenye mazingira yenye hewa ya kutosha. Kwa kufanya mazoezi kila siku na yale ya kuvuta pumzi na kutoa, hudhoofisha saratani.
Wakati mgonjwa wa saratani akijiepusha na ulaji wa vyakula vilivyoainishwa hapo juu, ulaji wa juisi za mboga na matunda na ulaji wa mboga za majani za aina mabilimbali, huwa ni wa lazima na endelevu, lengo likiwa ni kupunguza makali ya saratani.

2 comments:
hapo kwenye sukari mtihaniii, nyama mtihaniii, maana wa TZ wengi tumefanya nyama ni chakula cha Tunu, samaki ikaonekana ni kitoweo cha kawaida tu.
Jamani tule dagaaaa kwa afya. asante sana kaka, leo umenipa darasa zuri sana.
swali: sasa maziwa tunaambiwa sisi watu tunaotumia computer kwa muda mwingi yanatusaidia, inakuwaje hapa kaka?
oh, darasa zuri sana, na hiliwangeliweka kwenye runinga, maredioni angalau lifikie watu wengi.Ahsante sana
Post a Comment