Monday, November 22, 2010

ALI KIBA USO KWA USO NA JK!

Msanii Ali Kiba anakuwa msanii wa kwanza wa Bongo Flava kukutana katika uwanja wa burudani na Rais JK tangu aapishwe kuongoza nchi katika awamu ya pili ya uongozi wake. Amekutana na JK na kupiga nae picha baada ya kufanya onesho live la wimbo alioshirikiana na wasanii wengine, Hands Across The world, wakati wa uzinduzi wa jina jipya la Airtel usiku wa leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
JK akimkumbatia Ali Kiba wakati akipiga nae picha
Madam Rita akiwa na AY
Lawarence Masha ana kwa ana na Mustapha Hassanali mbunifu wa mavazi nchini
mratibu wa kundi la ONE8 nchini Tanzania aliyefanikisha ushiriki wya Ali Kiba katika kundi hilo, Christine Mosha 'seven' kushoto, akiwa na rafiki yake.

No comments: