alam,
MAELFU ya wafuasi wa dini ya Sikh
walijitokeza siku ya Jumapili tarehe 6 Novemba 2011 katika mji wa
Southall, Middlesex UK ili kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi
wa dini yao Guru Nanak aliyezaliwa mwaka 1469 nchini Pakistan.
Wakati akiwa na umri wa miaka 30 alipotea kwa hali ya miujiza kwa muda
wa siku tatu. Alipo rejea alianza kuhubiri, kufundisha na kuandika dini
ya Sikh wakati wa maisha yake yote. Pia Guru Nanak alisafiri dunia nzima
kuitangaza na kujadili dini hii kwa waumini wengine kama waislamu
pamoja na Wahindu.
Kwa miaka zaidi ya 550 wafuasi wa dini hii wamekuwa na desturi hii ya
kusherehekea siku moja kabla ya kuzaliwa kwake Guru Nanak kwa kuandaa
maandamano haya makubwa ya Sherehe hii ambayo hufanyika India pamoja na
baadhi ya sehemu za nchi ya Uingereza.
Kwa kawaida sherehe hizi huongozwa na wafuasi wakuu watano
wanaojulikana kama "Panj Piare" wakiambatana na waimbaji, wanamuziki na
timu ya wacheza Upanga (Martial Arts) kuelekea hekaluni kwao "Gurdwara"
Sri Guru Singh Sabha, hapa Southall hekalu lao ndio kubwa kuliko yote
katika bara la ulaya.
Sherehe hizi huanza mapema asubuhi kwa kuimba, kuomba kwa pamoja.
Baadae chakula cha kitamaduni kinachojulikana kama "Langar" hutolewa
bure kwa kila mtu.
Maandamano ya Southall yanaitwa Nagar Kirtan,
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVE
Maandamano ya Southall yanaitwa Nagar Kirtan,
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVE
No comments:
Post a Comment