Saturday, December 10, 2011

Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) kuzinduliwa rasmi Leo

 Kikosi Kazi cha Ngoma Africa band aka FFU,kimeshatua mjini Berlin kwa kazi moja tu, nayo ni kushambulia na muziki wake katika kusherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.

Kuanzia 9 hadi 10-Dec-2011 mjini Berlin ambako ndipo hupo Ubalozi wa Tanzania na ndio mji mkuu wa Ujerumani,kutakuwa hapatoshi kwani sherehe hizo zitaambatana na ufunguzi wa UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU) siku ya jumamosi 10-12-2011,umoja huo unawaunganisha watanzania wote waishio ujerumani,ulitiliwa nguvu na balozi Mh.Ngemera, umeshasajiliwa na viongozi wake ni Bw.Mfundo Peter Mfundo(mwenyekiti) na Bi.Tullalumba Mloge (katibu),utaratibu unaonyesha kuwa sherehe hizo mjini Berlin zitaanza saa 9 mchana  hadi usiku usio kwisha ambapo Ngoma Africa Band aka FFU,watatumbuiza na muziki wao,mahala patakapo fanyika sherehe Apostelkirche 1, 10738 Berlin,

UMOJA NI NGUVU WATANZANIA JITOKEZENI ! KUSHREKEA MIAKA 50 YA UHURU !
sikiliza muziki at www.ngoma-africa.com

No comments: