Je ?unajua kuwa hadithi za Filamu zozote hujengwa kwa wahusika, wahusika ndiyo
wabeba lengo zima la filamu? je wajua jinsi ya kuwajenga wahusika wako ili waweze
kubeba lengo la hadithi ya Filamu kiufasaha? je unajua kuwa ukikosea kumjenga
mhusika mkuu katika hadithi ya Filamu yako ni vigumu hadithi ya Filamu bora? basi
ukitaka kuyajua yote haya karibu katika warsha ya uandishi wa miswada ya filamu
pale IDARA YA SANAA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM Kuanzia tarehe 13-15
Februari 2012 ,Kutakuwa na Warsha ya Uandishi wa Miswaada ya Filamu/Screenplay
Workshop(Level 1) , Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho, Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam kila siku kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana , Cheti cha Ushiriki
kitatolewa mwishoni mwa mafunzo.
Warsha itakuwa kwa Kiswahili (na Kiingereza ikibidi) na mshiriki anaweza kuwa mtu
yoyote anayependa kuandika miswada ya filamu (amateur scriptwriter) au mwandishi
anayechipukia (upcoming scriptwriter)
Hima wadau wote wa Tasnia ya Filamu ,Sanaa, Sanaa za Maonyesho na Uandishi wa
ubunifu msikose nafasi hii muhimu ya warsha mafunzo daraja la kwanza ilikujijengea
misingi mizuri ya Uandishi wa Miswaada ya Filamu
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na warsha hii tafadhali wasiliana na IDARA YA SANAA
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM ,Ndg.John Mwakilama Simu Namba 0714 13 22
49, na barua pepe :mwakilamajohn@yahoo.com
2 comments:
Kipaji ni lazima kiboreshwe ili uwe bora zaidi,kwani kipaji pekee hakitoshi kukufanya uwe bora
ukitaka kujifunza kuandika miswada ya filamu kwa lugha ya kiswahili kinachoeleweka tembelea bongofilm.host.org
Post a Comment