Thursday, March 22, 2012

Askari Polisi Ashinda Milioni 10 za M-PESA

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza(kushoto)akimkabidhi
mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 mshindi wa mwezi wa
promosheni ya M-PESA Peter Kilalo.Katikati ni Ofisa Mkuu wa M-PESA Dylan
Lenox. Jumla ya shilingi milioni 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo
inayoendelea inahusisha pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na
nyongeza ya hadi asilimia 25 mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya
M-PESA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza wapili toka kushoto
akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani,wakati wa kumkabidhi mfano wa
hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10 mshindi wa mwezi wa promosheni ya
M-PESA Peter Kilalo watatu.kulia ni Ofisa Mkuu wa M-PESA Dylan Lenox,kushoto
Ofisa Mkuu wa Mahusiano na Biashara Mwamvita Makamba. Jumla ya shilingi
milioni 480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea inahusisha
pia punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia
25 mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na waandishi wa habari
wakifatilia makabidhiano ya mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 10
kwa mshindi wa mwezi wa promosheni ya M-PESA Peter Kilalo.aliyokabidhiwa
rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza.Jumla ya Milion
480 zinashindaniwa katika Promosheni hiyo inayoendelea inahusisha pia
punguzo la gharama katika utumaji wa fedha na nyongeza ya hadi asilimia 25
mteja anaponunua muda wa hewani kwa njia ya M-PESA.
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imemkabidhi hundi mshindi wa zawadi ya
kitita cha Shilingi Milioni Kumi wa droo ya mwezi ya promosheni ya M-PESA Bw
Peter James Kilalo.

Bw. Kilalo amekabidhiwa hundi hiyo leo jijini Dra es salaam na Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacoim Tanzania Bw. Rene Meza katika hafla fupi iliyohudhuriwa
pia na waandishi wa habari.

Akipokea hundi yake Bw. Kilalo ambae ni Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama
Barabarani Kituo Kikuu cha Dar es salaam ameshukuru kw akuibuka mshindi
jambo ambalo amesema hakulitegemea.

"Kwa kweli mimi ni mteja mzuri sana wa M-PESA lakini kweli sikutegemea
kwamba ningeibuka mshindi, ila sasa ninapopokea hundi hii naamini kwamba
nimeshinda na fedha hizi Milioni kumi ni zangu"Alibainisha Bw. Kilalo.

Alipoulizwa namna alivyojipanga kutumia pesa hizo Bw Kialalo alijibu" Jamani
mimi ni masikini na sikuwahi kuota kwamba ipo siku nitashinda kiasi kikubwa
cha fedha namna hii hivyo jambo kubwa kwangu kwa wakati huu ni kwanza kuacha
akili yangu itulie kabisa ndio niamue niziwekeze wapi ili zinikwamue
kimaisha"Alisema

"Nina mawazo kadhaa ya biashara ambayo nimekuwa nikiyawaza kama njia ya
kutafuta namna ya kujikwamua kimaisha hivyo hizi pesa nitazielekeza huko ila
baada ya akili yangu kwanza kutulia kutoka katika hali ya furaha niliyonayo
sasa."Aliongeza

Mshindi huyo ametumia pia fursa hiyo kuwashauri watanzania kutumia huduma ya
M-PESA kwa kuwa mbali na kwamba imerahisisha maisha katika utumaji na
upokeaji fedha mijini na vijijini bado wanaweza kuwa katika nafasi ya kushinda kama yeye

Awali  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza amesema promosheni hiyo
imelenga kuwawezesha wateja wa M-PESA kubadili masiha kutokana na
wanavyotumia huduma hiyo.

"Promosheni hii tulizindua mwezi uliopita tukilenga kuwawezesha wateja wetu
kujishindia zawadi za fedha taslimu, kiasi cha Shilingi Milioni 480
kinashindaniwa ambapo hadi sasa wateja zaidi ya 4,000 wameshajinyakulia
zaidi ya Shilingi Milioni 120" Alisema Bw. Rene

AmesemaVodacom inatambua umuhimu wa huduma ya M-PESA katika maisha ya kila
siku ya wananchi na hivyo wakati wote imekuwepo mikakati imara ya kuiwezesha
huduma hiyo kuendelea kuwa bora zaidi,salama na ya kuaminika sokoni.

"Matumizi ya huduma ya M-PESA hapa nchini yamekuwa yakiongezeka kwa kasi
sana, kiwango cha wananchi kutuma na kupokea pesa pamoja na kufanya malipo
ya bidhaa mbalimbali kupitia M-PESA ni kikubwa jambo ambalo linakuwa rahisi
zaidi kutokana na mtandao mpana tulionao wa mawakala wanaofikia 20,000
mijini na vijijini." Aliongeza Bw Rene

Promosheni hiyo itadumu kwa siku tisini kutoka Februari 13, 2012 hadi May
13, 2012. Mbali na kutoa mshindi mmoja wa shilingi milioni kumi kila mwezi
pia kila siku washindi mia moja hujishindia Shilingi 50,000 kila mmoja.

No comments: