Friday, March 23, 2012

KUFUNGWA KWA MASHINDANO YA UCHORAJI NA KUTOA ZAWADI

Siku ya Jumamosi tarehe 24/03/2012 kutakuwa na kufungwa na kugawa
zawadi kwa washindi wa Mashindano ya Uchoraji yaliyobeba kichwa cha
Habari cha Miaka 50 ya Taifa yakishindanisha Tasisii za Elimu kuanzia shule
za awali ,Msingi,Sekondari na Vyuo ,mashindano yaliyoandaliwa na Image
Profession.

Hafla ambayo itatanguliwa na maonyesho ya picha za washiriki wa
shindano pamoja na kuonyesha picha za wachoraji wazoefu kuanzia saa
11 :00 (Saa Tano)asubuhimpaka saa 14 :00(Saa Nane)Mchana kwenye
Ukumbi wa Jumba la Makumbusho ya Taifa makabala na Chuo cha
Fedha(I.F.M.)

Njoo ushuhudie Vipaji katika Sanaa za Uchoraji ,njoo uwape moyo
Washiriki na pia uweze kujifunza mambo mengi yahusuyo sanaa hii ya
uchoraji.

Pia Njoo ujuwe kichwa cha habari cha Mashindano ya Mwaka huu 2012.

WENU KATIKA UJENZI WA SANAA NA MICHEZO

Image Profession & iP Sports Club

22/03/2012

No comments: