Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja (kulia) amekutana na
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bw. Alberic Kacou ofisini kwake
jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuelekea Dodoma ambapo vikao vya Bunge
vinaendelea.
Mh. Ngeleja amekutana na Mwakilishi huyo baada ya kuwasili
kutoka katika mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa unaohusu
Nishati uliofanyika nchini Ubelgiji.
Mh. Ngeleja aliiwakilisha Tanzania katika sekta ya Nishati
ambapo Umoja wa Mataifa unategemea Nishati kuwafikia watu wote ifikapo Mwaka
2030.
Mh. Ngeleja amesema kuwa pamoja na changamoto zilizopo haswa
upatikanaji wa fedha, Serikali ya Tanzania imedhamiria kusambaza nishati nchini
Tanzania (yenye watu zaidi ya milioni 45) kutoka asilimia 18.5 hadi asilimia 30
ifikapo mwaka 2015.
Naye Mwakilishi wa Umoja wa Matifa amemshukuru Waziri kwa
jitihada zake kupitia wizara hiyo na akasisitiza kuwa Nishati kwa kila mtu ni
haki ya msingi hivyo uharakishwaji wa mpango huo wa nishati kwa wote upewe
umakini mkubwa.
Pia ameahidi kufikisha maombi ya Waziri wa Nishati ikiwa ni
pamoja na kuondolewa vikwazo vya upataji wa fedha kwa nchi zinazoendelea
ikiwemo Tanzania kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon.
Kusoma zaidi: http://tz.one.un.org
Imetolewa na Ofisi ya
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa – Afisa Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment