Thursday, May 3, 2012

WAZIRI WA HABARI AZINDUA MUUONGOZO NA KANUNI KWA WAMILIKI NA MAMENEJA WA VYOMBO VYA HABARI

 
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abdalah Mrisho (wa pili kushoto) na waratibu wenzake wa  mkutano huo wakiandaa mazingira kabla ya mkutano huo kuanza.
 
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Chama Cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (Moat), Reginald Mengi, akifungua mkutano huo.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi, akitoa hotuba na kuwasifu wamiliki wa vyombo vya habari nchini kwa kuamua kwa hiyari yao kuanzisha muungozo huo.
 
Waziri Nchimbi akiweka saini makubaliano hayo na Mwenyekiti wa Moat, Reginald Mengi (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya kuendeleza Vyombo vya Habari Afrika (AMI), Amadou Mahtar Ba.
 
Wakijadiliana jambo baada ya kutiliana saini makubaliano hayo.
 
Waziri Nchimbi na Mengi wakiwa na nyuso za furaha wakati wakiteta jambo.
 
Mwenyeki wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akichangia mada wakati wa mjadala wa kuboresha taaluma ya habari.
 
Mwanasiasa  maarufu nchini, Prince Bagenda naye akichangia hoja.
 
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya uzinduzi wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka kulia, Henry Muhanika (Katibu), Masoud Sanani (Mjumbe), Abdallah Mrisho (Mjumbe), Theophil Makunga (Mwenyekiti) na Hamza kasongo (mjumbe). 
Mwenyekiti wa Moat, Reginald Mengi, akiongea na wanahabari baada ya kutiliana saini makubaliano hayo.
 
Ulipowadia wakati wa maakuli.
Wamiliki na mameneja wa vyombo vya habari nchini leo wametiliana saini mbele ya  Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi, makubaliano ya hiyari ya kuanzisha na kulinda Muungozo na kanuni za kuendesha vyombo vya habari nchini na nchi zingine barani Afrika. Makubaliano hayo yalisainiwa kwenye mkutano wa uzinduzi uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huyo mijadala mbalimbali ya kuboresha taaluma ya habari ilijadiliwa.

                                

No comments: