Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akifafanua kuwa Tanzania kama mwanachama
wa mkataba wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabianchi amesema
Tanzania imeandaa Rasimu ya Ripoti ya Rio+20 itakayojadiliwa na mkutano
huo.
Bw.
Muyungi alitumia fursa hiyo kuwakilisha mada kuhusiana na maendeleo
endelevu ya Tanzania katika miaka 20 tangu mwaka wa kwanza kufanyika
mkutano wa kwanza wa RIO iliyohusu "wapi tulipokuwa na wapi tulipo
sasa". Bw.
Muyungi ameongeza kusema kuwa Mkutano huu utaainisha hatua
zitakazoangalia utekelezaji na kuhuisha nguzo zote tatu za maendeleo
endelevu (mazingira Uchumi na Jamii) kwa kufuata kanuni za usawa huku
tukitambua tofauti katika uwajibikaji na uwezo.
Upatikanaji
wa njia mpya, za ziada, thabiti, zinazotabirika za kupata fedha kwa
ajili ya kutekeleza shughuli za usimamizi wa mazingira na maendeleo
endelevu kwa nchi zinazoendelea.
|
No comments:
Post a Comment