Msanii
chipukizi wa Injili hapa nchini Eveline Kabwelile anategemea kuachia albamu
yake ya kwanza aliyoibatiza jina la YESU KOMANDO yenye jumla ya nyimbo tisa
aliyoirekodi katika studio ya Iki Production chini ya Producer Iki
1. Yesu komando
2. Ananitosha bwana
3. Mungu hawezi kukusahau
4. Nakupenda mokozi
5. Mshukuru Mungu
6. Ni wewe mwenyewe
7. Usinipite Mokozi
8. Mokozi asifiwe
9. Ni nani
Albamu
hiyo inategemewa kuzinduliwa tarehe 12 may 2013 katika Kanisa la Hollyness
pentecote kwa Mchungaji Ndalima
Ubungo kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi na mbili jioni.
Akizungumzia
sababu hasa iliyomfanya kuingia kwenye uimbaji wa Nyimbo za injili Eveline
amesema kwa upande wake anasukumwa sana na wito wa Mungu kwani nilianza kupenda
kuimba toka nikiwa mdogo na iko kwenye damu, yake
“Nilianza
kuimba toka nikiwa mdogo sikumbuki ni mwaka gani, albamu hii nimeanza akuiandaa
2010 na 2011 ndio nikaanza
kurekodi audio za nyimbo zangu na nilianza kurekodi video za nyimbo zangu mwaka 2012 katika
studio Brayanz work chini Byayan Hasani na nyimbo zote zimeshakamilika audio na
video tayari kwa uzinduzi”
Albamu
ya audio na video ya albamu Yesu Komando itaanza kuuzwa siku ya uzinduzi
No comments:
Post a Comment