Kilele
cha tuzo za Muziki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Music Awards
kinatarajia kufanyika siku ya Jumamosi, Juni 8 katika ukumbi wa Mlimani
City kwa kuwapa tuzo wasanii waliofanya vizuri katika kipindi cha mwaka
2012. Kwa mara ya kwanza mwaka huu kutakuwa na tukio la Red Carpet
ambapo watu maarufu watapita kupiga picha na kufanya mahojiano ya moja
kwa moja na muendeshaji ambaye ni mtangazaji wa kituo cha Channel O,
Jokate Mwegelo.
Tuzo
hizi zitaonyeshwa live kupitia katika mtandao wa Internet huku
watumiaji wa simu za mikononi na kompyuta wasioweza kufuatilia kupitia
TV zao wakiweza kutazama mtandaoni katika ukurasa wa Facebook wa
Kilimanjaro Premium Lager (www.facebook.com/kilimanjaropremiumlager) na pia mtandao wa LIVESTREAM (http://new.livestream.com/KTMA2013/live)
. Wakati wa zoezi la utoaji tuzo washindi wote watapata nafasi ya
kuongea na kuwashukuru mashabiki katika Social Media Lounge
itakayoendeshwa na Millard Ayo kutoka Clouds FM na Sam Misago kutoka
East Africa TV. Picha za matukio na kinachoendelea katika ukumbi wa
Mlimani City zitakuwa zikirushwa moja kwa moja katika mtandao wa Twitter
na Instagram ambayo ni ( @Kili_Lager).
No comments:
Post a Comment