Tuesday, July 30, 2013

MWANDISHI WA HABARI JACLINE AAGWA NA KUZIKWA LEO KITANGILI JIJINI MWANZA

Marehemu Jackline Wanna Since 1970 - 23/07/2013.
Mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari mwanamama Jacline Wanna umeagwa leo nyumbani kwake eneo la Nyamanoro, kisha ukazikwa katika makaburi ya Kitangiri jijini Mwanza
Mwandishi wa Habari Leo Grace Chilongola akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Jacline Wanna.
Wakijumuika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Jacline Wanna ni safu ya waandishi wa habari mbele ni Novatus Makongo
Heshima kwa mwili wa marehemu zikiendelea.
Sitta Tuma akitoa heshima kwa mwili wa marehemu Jacline Wanna.
Radio Maria nayo iliwakilishwa.
Mwili wa marehemu ukitolewa nyumbani kwake kuelekea mazikoni.
Majira ya saa 9 na dakika kadhaa msafarakuelekea makaburi ya Kitangiri.
Ni katika eneo la makaburi ya Kitangiri.
Mwili wa marehemu ukishushwa kwenye nyumba yake ya milele.Mwenye fulana nyeusi na maandishi mgongoni ni mwandishi wa habari wa kampuni ya Global Publishers. Mashaka Baltazar.
Mashuhuda.
Uliumbwa kwa udongo na mavumbini utarudi.
Shukurani za MPC ziliwasilishwa na Makamu Mwenyekiti Mr. Mpagaze
Salamu za UTPC ziliwasilishwa na Victor Maleko.
Katibu wa Mwenezi wa CCM Wilaya ya Nyamagana Mr. Mustapha aliwakilisha salamu za Chama cha mapinduzi.
Waandishi wa habari wakiweka maua kwenye kaburi la hayati Jacline Wanna.
Wakiweka mashada ya maua kwenye nyumba ya milele ya mpendwa wao.


Hawa ni watoto wa marehemu aliowaacha.
Mara baada ya hatua za mazishi kukamilika mume wa marehemu katikati (mwenye kauda suti nyeusi) alijumuika na nduguze katika sala.

No comments: