Monday, October 7, 2013

UN HABITAT DAY



MIPANGO NA UBUNIFU
ENDELEVU WA UHAMAJI MIJINI:
 TAARIFA YA DUNIA KUHUSU MAKAZI YA BINADAMU 2013
Imewasilishwa na Bw. Phillemon Mutashubirwa
Mwakilishi wa UN Habitat, Tanzania, Katika kuadhimisha siku ya makazi Duniani 7 Oktoba 2013

Top of Form
Kwa zaidi ya nusu karne, nchi zina  uzoefu wa ukuaji wa  haraka wa uchumi mijini  na kuongezeka kwa matumizi ya vyombo vya moto(k.m magari,pikipiki n.k). Hii imesababishwa na ukuaji holela wa  miji na mahitaji makubwa kwa ajili ya usafiri wa vyombo vya moto ambao una madhara mbalimbali  kimazingira, kijamii na kiuchumi.
Usafiri wa vyombo vya moto mijini ni chanzo kikubwa cha uzalishaji wa hewa ya ukaa ambayo inasababisha magonjwa kutokana na uchafuzi wa hewa, ajali zisizotarajiwa, msongamano na kelele n.k. Msongamano unaotokana na usafiri usio na mifumo endelevu ni wa  gharama kubwa kiuchumi na hauna tija kwa wasafiri  na bidhaa wanazosafirisha.

Changamoto hizi, nyingi tunazikuta katika miji ya nchi zinazoendelea.
Toleo la mwaka huu la Ripoti ya UN-Habitat ya Makazi ya Binadamu duniani inatoa mwongozo juu ya kuendeleza mifumo endelevu ya usafiri mijini. Ripoti hii pia inaeleza mwenendo,  hali ya mwelekeo na changamoto ya usafiri mijini na duniani kote.
Katika ripoti hiyo umefanyika  uchambuzi wa mahusiano kati ya mfumo wa miji na uhamaji, na unatoa wito kwa ajili ya miji ya kisasa inavyostahili kuwa hapo baadaye. Inaonyesha jukumu la mipango miji katika kuendeleza miji endelevu ambapo usafiri wa umma usiokua wa vyombo vya moto unapendelewa zaidi.

Ripoti inatoa  mapendekezo namna gani taifa, mikoa na serikali za mitaa na wadau wengine wanavyoweza kuweka mipango ya kuboresha na kubuni usafiri endelevu mijini ili kupata nafuu sio kwa usafiri tu, bali pia katika kutoa huduma, kuuza na kununua bidhaa zetu .
Makusudi mazima ya usafiri na uhamaji ni kufika unapotaka kwenda, lakini iwe kwa bei  nafuu na bila kuleta madhara. Ujenzi wa barabara zaidi kwa ajili ya miji ya nchi zenye kipato cha chini ni muhimu sana katika kutafuta suluhu la ufumbuzi wa usafiri endelevu, kwa hiyo ni muhimu sana watu wa  mipango miji kubuni miji itakayo zingatia upatikanaji wa huduma zote sehemu moja, hivyo kupunguza umbali wa kusafiri na kuongeza upatikanaji endelevu wa usafiri mijini.  kwa mfano kama wakazi wa mijini wanaweza kufikia upatikanaji wa huduma wanazohitaji bila kusafiri mbali au kupata huduma hizo kupitia mitandao (mobile phone,online shopping) itasaidia kupunguza changamoto za usafiri mijini. Ubunifu wa miji iliyo mchanganyiko kimatumizi (mixed land use) italazimu halmashauri na serikali za mitaa zijenge miundombinu rafiki na muafaka, zitunge sheria na kanuni za kuhakikisha watu wanaishi na kufanya kazi karibu na maeneo yao.

Uwekezaji katika usafiri endelevu mijini ni muhimu hasa katika nchi zetu zinazoendelea, ambapo idadi kubwa ya watu hawawezi kumudu kulipa nauli inayohitajika kutumia usafiri wa umma, au kununua baiskeli. Wengine wanaweza kumudu njia hii ya usafiri wa gharama nafuu, lakini si chaguo lao kwa sababu mbalimbali, kwa mfano ukosefu wa miundombinu sahihi na usalama wakati wa kuendesha baiskeli.  Uwekezaji katika miundombinu kwa ajili ya vyombo vya moto vilivyo nafuu ( na kukubalika),tukiwa na mifumo mizuri ya barabara usafiri wa umma ni sahihi zaidi (na endelevu) na mwisho wa siku hutumia fedha chache.
 
Hata hivyo nchi nyingi duniani zinapata matatizo makubwa ya kitaasisi, kisheria na kiutawala zinapotaka kukabiliana na changamoto za uhamaji mijini. Katika kushuhulikia changamoto hizi ripoti inabainisha umuhimu wa kuhusisha wadau wote katika usafiri mijini (kama ngazi zote za serikali, watoa usafiri na waendeshaji, sekta binafsi, asasi za kiraia na watumiaji usafiri) kushiriki katika utawala na maendeleo ya mifumo ya uhamaji mijini.
Ili kuleta ushirikiano wa usafirishaji na sera za maendeleo ya miji ni muhimu kuoanisha usafiri mijini na sera za matumizi ya ardhi [mixed landuse].

Mahitaji ya usafiri mijini ni makubwa kuliko kiwango cha uwekezaji katika mifumo ya usafiri, Naamini ripoti hii itatumika kama mwongozo kwa serikali za mitaa  na wadau wengine katika kukabiliana na  changamoto za mifumo ya usafiri mijini na duniani kote. Mwisho, ripoti hii inatoa ufahamu na mawazo ya kuchochea ni jinsi gani tunaweza kujenga miji ya baadae itakayokua na mifumo endelevu ya usafiri mijini, itaboresha kumfikisha mtu anapotaka kufika na kutoa huduma nzuri kwa wakati mfupi inavyowezekana.

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA!






No comments: