Saturday, July 26, 2014

KIPINDI CHA “MIMI NA TANZANIA” CHAVUKA MIPAKA YA TANZANIA, SAFARI NI NDANI YA JIJI LA WASHINGTON DC

IMG-20140725-WA0004
Pichani ni Mtangazaji anayeongoza Kipindi cha 'Mimi na Tanzania' Hoyce Temu aliyewahi kushika taji Miss Tanzania mwaka 1999 akiwa nje ya Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani mara baada ya kuwasili ambapo alimua kufunga safari kwa ajili ya kufanya mazungumzo maalum na Balozi wetu wa Tanzania nchini Marekani Mh. Liberata Mulamula.
IMG-20140725-WA0006
Mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani.
IMG-20140725-WA0005
Hapa akiwa mapokezi ya Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani huku akisema ...Naipenda Tanzania yangu!
IMG-20140725-WA0003
Hoyce Temu akiangalia baadhi ya picha za Mabalozi 15 ambao tayari wameshaongoza Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani. wakiwemo Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, Mustafa Nyang'anyi na Balozi Ombeni Sefue pamoja Wanawake wawili ambao ni Mama Balozi Mwanaidi Maajar na Balozi wa sasa Mh. Liberata MulaMula.
IMG-20140725-WA0007
Mheshimiwa Balozi Liberata MulaMula ndani ya mahojiano na mtangazaji wa kipindi cha Mimi Na Tanzania Hoyce Temu ofisini kwake jijini Washington DC, Marekani!
Mahojiano hayo ya moja kwa moja katika Balozi ya Tanzania nchini Marekani na Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula ambapo wameangazia masuala mbalimbali yakiwemo Utalii, kujitangaza katika miradi ya kimaendeleo na uwekezaji ,malalamiko ya watanzania waishio Marekani kuhusu uraia, kwa mengineyo mengi usikose kuangalia Channel Ten wiki ijayo Jumapili saa moja na nusu usiku kilicho bora kabisa.
IMG-20140725-WA0009
Na wale waliokuja kuomba Visa wakapiga picha na aliyewahi kuwa mrembo wa Tanzania na muongozaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu.
IMG-20140725-WA0008
Hoyce Temu akipata picha ya ukumbusho na mpiga picha Iska JoJo aliyerekodi kipindi hicho.
Hoyce Temu anatoa shukrani za pekee kwa Blogger Mzee wa VIJIMAMBO DJ Luke Joe kufanikisha mahojiano ya Hoyce Temu na Balozi Liberata Mulamula.

NEW AUDIO: NIMEMPATA - PAM D MIC QUEEN FT MESEN SELECTOR

MANISPAA YA KINONDONI YAWAFUKUZA WATUMISHI TISA NA WENGINE WAWILI WAPEWA KARIPIO KALI

i

Friday, July 25, 2014

MKUTANO KATI YA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM NA WANAMTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA NA TAMWA LEO

 Usu Millya Mwanamtandao wa Ulingo wa Katiba na wanawake ambaye alikuwa ndiye mwezeshaji wa Mkutano huo ambao  ulikuwa ni wa siku mbili akiendelea kutoa mwongozo wa mkutano huo.
 Doreen E. Maro kutoka TAMPRODA ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba akiwakilisha Wafugaji Akileta Mrejesho wa walichokuwa wakikijadili katika Kundi lao juu ya mapendekezo ya kuimarisha Masuala muhimu ya Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya
 Dkt. Macca A. Mbalwa  Mkurugenzi wa Giyedo Tanzania akiwa anatoa Mrejesho wa kile ambacho walikuwa wamekijadili na kutoa mapendekezo yao ya Kuboresha masuala muhimu katika Rasimu ya pili ya Katiba Mpya.
 Salama Aboud Talib Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba  na Naibu Katibu Mkuu wa UWT akizungumzia makosa mbalimbali ambayo yapo katika Rasimu ya Pili ya Katiba mpya na kutoa mapendekezo kuwa Iboreshwe ili kuweka usawa.
 Executive Director wa  Women Fund Tanzania Mary Rusimbi akizungumza juu ya Majumuisho ya pomoja na Kupanga mikakati ambayo yatasaidia Kuimarisha Masuala Muhimu ya Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya
 Mgeni Hassan Juma Mwenyekiti wa Wawakilishi  Wanawake Zanzibar akitoa neno la Shukurani kwa wote waliohudhuria kwa muda wa siku mbili katika mkutano wa Wajumbe wa Bunge Maalum la  Katiba, Mtandao wa wanawake na TAMWA
 Profesa Ruth Meena  Akitoa Majumuisho pia kutoa Shukurani kwa wale wote waliohudhuria katika Mkutano huo uliochukua siku mbili.
 Valerie Msoka akifunga Rasmi Mkutano huo.
 Fredrick Msigala Mjumbe Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mlemavu wa Miguu akielezea masikitiko yake ya Jinsi watu wenye ulemavu wakiwemo wanawake na wanaume ambavyo wametengwa na kukosa haki zao, amesisitiza Serikali katika Rasimu Mpya ya Pili ya Katiba wawaangalie walemavu kwa umakini na ukaribu maana wanahaki sawa na watu wengine. Pia amesisitiza walemavu wajaliwe katika huduma za Afya mana ni Muhimu kwao. Mwisho amesisitiza kuwa wanawake wenye ulemavu wanahaki ya Kuolewa na kuto nyanyaswa pindi wanapokuwa katika ndoa zao.
 Modesta Mpereme ambaye ni Kiziwi hasikii lakini anaongea vizuri pia ni Mwenyekiti kutoka  Sauti ya Wanawake  wenye Ulemavu Tanzania, Ameiomba serikali iwe na vitendea kazi vya kutosha ambavyo vitawasaidia walemavu katika secta mbalimbali Mfano katika Mabenki kuwe na vifaa maalum vya kuwasaidia walemavu, Katika Upande wa Afya amesisitiza kuwe na hata watu wanaoweza kutoa msaada wa kutafsiri mambo mbalimbali mfano kwa Viziwi, wasio ona na ambao Hawawezi kuongea.
 Siti Ally Mwanasheria na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Zanzibar akisisitiza umuhimu wa usawa kati ya haki za wanawake na wanaume katika jamii , Pia alisisitiza juu ya mabinti wanaopata Mimba za utotoni wakiwa mashuleni na kusisitiza kuwa wanaruhusiwa kusimama masomo mpaka kipindi mtoto atakapokuwa mkubwa anaruhusiwa kuendelea na masomo,  Mwanaume aliyesababisha Mimba anaweza akashtakiwa .
 Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba pamoja na Wadau mbalimbali waliofika katika Mkutano huo.

TUJUMUIKE PAMOJA LEO KUCHEZA WIMBO MPYA WA SKYLIGHT BAND

Na hii ndio Video ya Skylight Band ya Wimbo mpya "PASUA TWENDE"
DSC_0078
Mary Lucos akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) huku akipewa sapoti na Hashim Donode sambamba na Digna Mbepera Ijumaa iliypoita kwenye viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0099
Vijana wa Skylight Band wakijimwaga na sebene, kutoka kushoto ni Joniko Flower, Sony Masamba na Sam Mapenzi.
DSC_0102
Sio kwamba wanaanguka la hasha ni mbewembwe za Majembe ya Skylight Band katika kutoa burudani kwa mashabiki wao.
DSC_0118
Mdau aliguswa na uchezaji wa wanamuziki wa Skylight Band na kuchomoa bulungutu la mapesa na kuwatunza wote watatu kama inavyoonekana pichani.
DSC_0126
Jukwaa likiwa limetapakaa manoti ya tanotano na wekundu wa msimbazi.
DSC_0175
Aneth Kushaba AK 47 a.k.a Komando Kipensi akishambulia jukwaa huku Digna Mbepera akitoa sapoti ya Back Vocal.
DSC_0181
I'm not worried 'bout a thing...Cause I know You are guiding me...Where You lead me, lord, I will go..I have no fear cause I know who's in control....Swagga za Aneth Kushaba AK47 njoo leo tuburudike na kuimba pamoja.
DSC_0170
Mashabiki wakijiachia na burudani ya nguvu kutoka kwa vijana wa Skylight Band ni kila Ijumaa kuanzia saa tatu kamili ndani ya kiota cha maraha cha Thai Village.
DSC_0144
Sam Mapenzi akipewa tano na wanafunzi wa CBE waliofika kwenye viwanja ya Thai Village kupunguza stress za mitihani yaliyomaliza hivi karibuni.
DSC_0159
oohhh na na na na....ye ye ye ye ye...oohhh na na na na...ye ye ye ye ye....oohhh na na na na...ye ye ye ye ye..oohhh na na na na...ye ye ye ye ye..Watoto wa CBE kwa raha zao wakijiachia.
DSC_0187
Hapo sasa twende kazi kwa raha zetu.
DSC_0212
Joniko Flower akiongoza kikosi cha Skylight Band kushambulia jukwaa.
DSC_0256
DSC_0224
Rais wa WANAMANYOYA Justine Ndege akimwaga manoti kwa vijana wake kama motisha kwa kazi nzuri wanayoifanya.
DSC_0228
Mguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma....Yachuma chuma ndio mpango mzima, Tukutane baadae ndio kitaeleweka zaidi.
DSC_0244
DSC_0234
Palifurikaje leo itakuwa zaidi ya jana.
DSC_0238
DSC_0278
Aneth Kushaba AK47 akiwajibika jukwaani.
DSC_0264
Warembo wa CBE wakijiachia kwa raha zao.
DSC_0191
Back stage...Mary Lucos na Digna Mbepera wakipata Ukodak na shabiki wao.
DSC_0074
Aneth Kushaba AK47 akiwa na mashabiki wake wanafunzi wa CBE wakipata Ukodak.
DSC_0076
DSC_0088
WANAMANYOYA wakipata Ukodak.
DSC_0093
Wadau wa Skylight Band wakipozi kwa Ukodak.
DSC_0091

Thursday, July 24, 2014

TABIA NA TAMADUNI HATARISHI ZINAZOCHANGIA MAAMBUKIZI YA VVU

DSC_0092
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akitoa mada kuhusu tabia hatarishi zinazochangia maambukizi mapya ua VVU kwa Vijana katika warsha ya siku tatu ya Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika katika Kituo cha Redio cha Nuru FM mjini Iringa.
Na Mwandishi wetu
Idadi kubwa ya Vijana hususan wa kike wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 wanaanza kufanya mapenzi katika umri mdogo jambo ambalo linaashiria hatari ya maambukizi ya VVU ikilinganishwa na idadi ya Vijana wa Kiume.
Akitoa mada kuhusu tabia hatarishi zinazochangia maambukizi mapya ua VVU kwa Vijana katika warsha ya siku tatu ya Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika katika Kituo cha Redio cha Nuru FM mjini Iringa, Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias, amesema hadi sasa kuna Asilimia 3.9 ya wasichana wenye umri huo wamepata maambukizi ya VVU ikilingaishwa na asilimia 1.7 ya wavulana.
Kufanya mapenzi pia katika umri mdogo kunachangia kwa kiasi kikubwa mimba za utotoni na kuathiri ustawi wa maisha ya wasichana. Wastani wa watoto wa kike 6,000 huachishwa masomo kila mwaka kutokana na mimba za utotoni.
DSC_0269
Mratibu na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akichangia mada iliyotolewa na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias (hayupo pichani) katika warsha ya siku tatu ya Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika katika Kituo cha Redio cha Nuru FM mjini Iringa.
“Wasichana wengi wamekatishwa masomo kwa ajili ya kupata Mimba za utotoni zinazochangiwa na kufanya mapenzi katika umri mdogo tabia ambayo pia inachangia maambukizi ya VVU”, alisema Bw. Mathias.
Amezitaja tabia nyingine hatarishi zinazochangia maambukizi ya VVU kuwa ni kuwa na wapenzi wengi kwa wakati mmoja, kuwa na wapenzi wenye umri mkubwa na ngono wenzi.
Nyingine ni matumizi duni na yasiyoendelevu ya Kondomu, kufanya ngono wakati umelewa, ngono kinyume na maumbile na ngono ya jinsia moja.
Akichangia suala hilo Mratibu na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu amesema tamaduni zinazoendelezwa katika jamii pia zinachangia kumuweka msichana katika kundi hatarishi la kupata maambukizi ya VVU.
DSC_0066
Afisa Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumbe akitoa mada ya Afya ya Uzazi kwa Vijana na mahusiano yake na maambukizi ya VVU wakati wa warsha ya siku tatu ya Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika katika Kituo cha Redio cha Nuru FM mjini Iringa.
Amezitaja tamaduni hizo ikiwa ni pamoja na kumbagua Mwanamke katika majukumu mbalimbali Kijinsia kutokana na tabia inayofundishwa na kutolewa kwa mtu kulingana na jinsi yake.
“Jinsia, Utamaduni na VVU ni masuala yenye mahusiano yanayomuweka Mwanamke katika hali ya hatarishi kupata maambukizi ya VVU, na kubadili tabia si jambo rahisi kwa sababu limejikita katika tamaduni zetu zinazoelekeza majukumu mbalimbali ya mwanamke na mwanaume kijinsia na hivyo kuchangia maambuki ya VVU” amesema Bi. Mwalimu.
Amesema ni jukumu la Wanahabari Vijana kuhakikisha kuwa wanahamasisha kubadilisha tabia hatarishi zinazochangia maambukizi ya VVU ambazo zimemzunguka mwanamke.
Baadhi ya mifano halisi ya kijinsia kwa wanaume na wanawake katika Afrika ikiwemo Tanzania ni kumuona mwanamume kama kiongozi katika kaya, jamii na kuwajibika kufanya maamuzi yote wakati mwanamke huonekana ni mlezi na kulinganishwa na mtoto mdogo.
DSC_0037
Mfano mwingine ni mitala. Mahusiano ya kimapenzi hata katika jamii isiyokumbatia mitala kutoka na tamaduni zilizojikita katika jamii inakubalika kwamba mwanaume ana haki ya kuwa na wapenzi wengi wakati wanawake wanatakiwa kuwa waaminifu kwa mtu mmoja ambao ni waume zao.
“Wanawake pia wanatarajiwa kuwa watiifu kwa waume zao lakini utiifu huo hautegemewi wapewe wanawake kutoka kwa waume zao. Wanawake watakaokwenda kinyume na kanuni hiyo hunyooshewa vidole na kuambiwa kuwa wazinzi na wanaweza kuadhibiwa na jamii kwa namna yoyote ile hususani kupigwa, kutolewa maneno makali na kupewa talaka lakini wanaume hawafanyiwi hivyo”.
Kutokana na tamaduni hizo yanajengwa mazingira ambayo mwanamke anakuwa hana uwezo wa kujadili masuala ya ngono salama au ya kuridhisha kwa sababu kunakuwa hakuna mawasiliano katika nyumba kuhusu ngono kati ya mume na mke.
DSC_0227
Mshiriki wa warsha hiyo Veronica Mtauka kutoka Kitulo FM Redio Makete akishiriki kuchangia mada wakati wa warsha hiyo.
Mradi wa SHUGA Redio unaotekelezwa kwa ushirikiano wa Mashirika ya Kimataifa moja linaloshughulikia Huduma za Watoto (UNICEF), Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Redio Jamii 10 nchini Tanzania una lengo la kuendeleza kampeni za hamasa kwa vijana kupunguza maambukizi mapya ya VVU.
Redio hizo ni kutoka Karagwe, Kahama, Kyela, Kitulo na Kwanza Jamii. Nyingine ni kutoka Iringa, Simanjiro, Ifakara, Sengerema na Uvinza.
DSC_0091
Mtangazaji wa Uvinza FM Redio, Mwinyi Mtulla akichangia hoja wakati wa warsha hiyo ya siku tatu inayoendelea mjini Iringa.
DSC_0200
Mratibu na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akiwaelekeza jambo baadhi ya washiriki wakati wa warsha hiyo inayoendelea kwenye kituo cha Redio Nuru FM mjini Iringa.
DSC_0027
Pichani juu na chini ni baadhi ya washiriki wa warsha ya siku tatu ya Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika katika Kituo cha Redio cha Nuru FM mjini Iringa inayolenga kuendeleza kampeni za hamasa kwa vijana kupunguza maambukizi mapya ya VVU.
DSC_0047
DSC_0016
DSC_0182
Baadhi ya washiriki kutoka Redio za Jamii mbalimbali watakaotekeleza Mradi wa SHUGA Redio wakiwa kwenye vikundi kazi.
DSC_0198