Mwenyekiti wa Chadema Freman Mbowe akiwa anasoma utuba wakati wa ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa chama hicho wa kanda ya kaskazini unaofanyika leo katika hotel ya new Arusha jijini hapa |
viongizo wa chadema akiwemo
mwenyekiti wakiwa wanasali kwanza kabla ya mkutano wa viongozi wakanda
ya kaskazini kuanza
Naibu katibu mkuu wa Chadema Salum Mwalimu akiwa anaongea nawaandishi
wahabari
MWENYEKITI wa chama cha demokrasi na maendeleo
Chadema Freeman Mbowe amesema kuwa chama chao kimejipanga
kuahakikisha kinahamasisha kwa nguvu zote wananchi weweze
kwenda kujiandikisha katika daftari la mpiga
kura
Alisemakuwa hii
itaweza kumsaidia kila mwananchi kuweza kupata haki yakumchagua
kiongozi bora anaemtaka katika uchaguzi mkuu
ujao wa kuwachagua viongozi wakuu ambao ni rais ,wabunge na
madiwani.
Alisema kuwa
pamoja ya kuwa tume wamekuwa wananchelewesha kufanyika kwa zoezi hili
, wao wamejipanga kikamilifu na pindi ambapo zoezi hili
litatangazwa kuanza rasmi watajitaidi kwa njia yoyote
kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi
kujiandikisha
Alisema kuwa kwa
upande wa kupiga kura katiba wanaendelea na msimamo wao ambao
walitangaza awali wa kutoshiriki katika mchakato wa kura
ya maoni ya katiba huku akisisitiza kuwa swala la kutoshiriki
katika mchakato wakura za maoni auingiliani kabisa na
kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga
kura
Alimaliizia kwa kuwasihi wananchi wajitokeze kwa wingi
sana pindi pale ambapo watasikia zoezi la kujiandikisha kwenye daftari
la kudumu limewadia ili waweze kupata haki yao ambayo
itawaruhusu kuchgua kiongozi wanao wataka.
No comments:
Post a Comment