Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa watu kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, akiendelea na kampeni zake za kuisaka Ikulu nchini Kote huku akiwaomba Watanzania kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ili aweze kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa.
Baadhi ya wananchi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake wakimsiiliza Dkt Magufuli alipokuwa akinadi sera zake za kuomba kura ili kushika nafasi ya Urais ya awamu ya tano.
Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, akimnadi Dkt.Magufuli kwa kuhubiri amani katika mikitano yake ya kampeni kuliko wagombea wa vyama vingine hawasisitizi kudumisha amani nchini jambo ambalo ni tunu ya taiafa
Dkt. Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa Dodoma Mjini,mara baada ya kumkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Ndugu Anthony Mavunde wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Jamhuri mjni Dodoma leo.
Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje,mjini MPwapwa katika uwanja wa mgambo.
Mgombea
urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimnadi Mgombea ubunge
Jimbo la Kongwa, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai wakati wa mkutano wa
kampeni jimboni humo.
Mawaziri wakuu wa zamani, John Samuel Malecela na Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Dodoma kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli, akimsimamia Mgombea ubunge Jimbo la Mtera kupitia CCM, Livingstone Lusinde aliyekuwa akifanya mazoezi ya Push Up wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akimuombea kura Dk Magufuli wakati wa mkutano huo wa kampeni mjini Dodoma jioni ya leo.
Walemavu nao wana haki ya kuwasikiliza Wagombea nafasi mbalimbali ikiwemo ya Urais,Ubunge na Udiwani
Wananchi wa Kibaigwa wilayani Kongwa, wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt. Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni mjini Kongwa.
Mgombea Urais Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu wa zamani Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba,mjini Kibaigwa wilayani Kongwa kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Wananchi wa Kibaigwa wilayani Kongwa wakifuatilia hotuba za Dkt Magufuli kwenye mkutano wa kampeni.
Dk Magufuli akijipigia kampeni kwa wakazi wa Kibaigwa , wilayani Kongwa leo.Akiwa wilayani Kongwa, Dk Magufuli amesema kuwa akishinda urais atahakikisha anadhibiti mapigano kati ya wakulima na wafugaji yanayoendelea nchini na kusababisha vifo vya watu wengi
Dkt. Magufuli akiwapungia mikono wananchi alipowasili kwenye kampeni Uwanja wa Jamhuri Dodoma leo.
PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA
PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA
Akitoa hotuba yake katika moja ya mikutano yake alioufanya katika mji wa Kibaigwa Dk. John Pombe Magufuli amesema hakuna kitu kinachomuumiza kama mauaji ya wakulima na wafugaji yanayotokea kati ya wilaya za Kongwa Mkoani Dodoma na Kiteto mkoani Manyara.
Dkt Magufuli ameahidi kuwa mara baada ya kuchaguliwa na kuunda Serikali yake,jambo hilo atalipa uzito wa juu na kulifanyia kazi kwa umakini mkubwa. “Yaani Mimi Magufuli Nimteuwe Waziri na watendaji wengine wa serikali halafu Mauaji yatokee watu wafe, Mkuu wa mkoa yupo , Mkuu wa wilaya yupo na Kamanda wa Polisi yupo wabaki wanapunga upepo, wamiliki wa Ng’ombe wabaki wanakula maisha haiwezekani,nitalala nao mbele na Ng’ombe wataliwa msibani kwa uzembe waliousababisha”,alisema Magufuli kwa msisitizo mkubwa.
Magufuli amewataka wafugaji na wakulima kuishi kwa amani bila kubaguana, lakini pia akasema atatumia sheria za ardhi na kuhakikisha maeneo ya wafugaji na wakulima yanatengwa, ili wafanye shughuli zao na kukuza kipato na uchumi wao bila kusumbuliwa.
No comments:
Post a Comment