Wednesday, November 18, 2015

Anania Ngoliga na John Kitime watambulisha muziki wao



Anania Ngoliga na John Kitime ni wanamuziki wa zamani ambao hufahamika zaidi kwa muziki wa Dansi. Anania ambaye alipoteza uwezo wake wa kuona akiwa bado mtoto mdogo, amewahi kupitia bendi kama Jambos na 
Afriso Ngoma ambapo alikuwa akiimba na mwanamuziki nguli Lovy Longomba akiwa na  wakali wengine kama Ramadhani Kinguti, kisha akapigia bendi ya Legho Stars akiwa na wanamuziki kama Joseph Mulenga (King Spoiler) na Tchimanga Assossa, na katika bendi hii licha ya kuimba pia alikuwa anapiga kinanda na gitaa. Akapitia bendi nyingine kama Ram Choc StarsLiving Light Band na VICO Stars za Iringa hatimae akajiunga na TACOSODE Band  ilipokufa akajiunga na Tango Stars na kwa sasa yuko Karafuu Band ya Zanzibar. John Kitime nae amepitia bendi kama Orchestra Mambo Bado iliyokuwa chini ya uongozi wa Tchimanga AssossaOrchestra Makassy, TX Seleleka, Tancut Almasi Orchestra ya Iringa ambako alikuwa jukwaa moja na Abdul Salvador, Kasaloo Kyanga na pacha wake, akina Kawelee, Kalala Mbwebwe na majina mengine makubwa katika historia ya muziki Tanzania, kisha Vijana Jazz akiwa Hemed Maneti , Jerry Nashon na wengine wengi , baadae Magoma Moto Sound na kwa sasa yuko na Kilimanjaro Band. Lakini wanamuziki wawili hawa wamekuwa na staili yao ya muziki ya peke yao, ambayo tayari wamekwisha jikuta wakifanya 'tour' mbili Marekani zilizowazungusha majimbo mengi ya nchi hiyo katika 'tour' zilizochukua jumla ya miezi mitatu, pia wakajikuta Mumbai India wakifanya maonyesho kupitia muziki wao huu. 
Kwa mara ya kwanza walifanya maonyesho ya aina ya muziki huu katika tamasha la Karibu lililokuwa Bagamoyo siku chache zilizopita na kufuatiwa na onyesho jingine katika jukwaa la Baraza liliokuwa Alliance France. Video hii iliyopigwa 'live' ni vionjo vya staili yao faidi utamu, kwa zaidi wasiliana kupitia anania.john@gmail.com au +255713274747

No comments: