Thursday, November 19, 2015

DKT KIGWANGALLA ATOA USHAURI WAKE JUU YA UDHIBITI WA MADAWA SERIKALINI


Dkt Hamisi Kigwangalla Mbunge Mteule Nzega Vijijini CCM.


Mbunge mteule jimbo la Nzega vijijini  Dkt Hamisi Kigwangalla  (CCM) ametoa ushauri kwa wizara husika juu ya udhibiti wa kuvuja kwa madawa serikalini na kwenda kwenye maduka binafsi.

Kupitia ukarasa wake facebook Kigwangalla amesema #‎SasaKaziTuChangamoto ya Udhibiti wa Kuvuja Madawa Kutoka Mfumo wa Serikali Kwenda Kwenye Maduka ya Watu Binafsi ni Katika Mambo ambayo mgombea Urais wa CCM, Ndg. John Pombe Magufuli alionesha kuwa yanamkera sana. Hivyo wananchi wanasubiri kuona nini kitafanyika kutatua changamoto hii...kuna 'expectation gap' ambayo ni lazima izibwe ndipo watu wasadiki kushuhudia #‎MabadilikoYaKweli.
Nimesikia kuna mkakati wa kutaka kuondoa maduka yote jirani na hospitali za serikali. Si wazo baya sana lakini ninaamini na ninajua kwa hakika kabisa kuwa kuna suluhisho bora zaidi ya hilo.
Inawashangaza watu wengi kuwa kwenye pharmacy za watu binafsi nje tu ya hospitali kuna dawa za kutosha za kila aina wakati kwenye pharmacy ya serikali ndani ya hospitali hakuna! Kuna watalamu wetu wanadhani suluhisho ni kuzuia uwepo wa pharmacy karibu zaidi na hospitali. Ninafahamu kwa mfano, kuna tafiti zimefanyika pale Muhimbili kuhusiana na idadi ya dawa zilizopo ukilinganisha na pharmacy mojawapo pale nje; matokeo ya utafiti huo yakawa, Muhimbili kuna dawa tofauti tofauti 850 (lines), wakati kwenye hiyo pharmacy kuna dawa tofauti tofauti takriban 3200!
Unaweza kusema si busara kuziondoa pharmacy hizi wakati tunajua kabisa kwenye hospitali yetu pale hakuna dawa za kutosha, maana itakuwa ni usumbufu kwa wagonjwa wanaoagizwa kutafuta dawa fulani ambayo Muhimbili haipo. Unaweza kusema kuwa aina mbalimbali zaidi ya 2300 za madawa zimeibiwa kutoka Muhimbili, na mimi hapo utanipa shida sana kukuelewa. Na nitakuuliza, zimepitia wapi pamoja na ulinzi uliopo? Na kama ziliwahi kuweza kutoka nje ya hospitali mpaka pharmacy, kwani pharmacy hiyo ikihamia Kariakoo ama Posta kutakuwa kuna ugumu gani wa 'wezi' hao wa madawa kuzifikisha huko pia kama wameweza kuzitoa?
Nadhani njia hii ni too 'mechanical' na haitoondoa tatizo zaidi ya kuzalisha tatizo lingine 'la usumbufu kwa wagonjwa'.
Nini kifanyike kudhibiti dawa zisikosekane kwenye mfumo wa afya?
1. Tuhakikishe tuna dawa za kutosha kwenye Idara ya Bohari ya Dawa (MSD) kwa kuongeza 'capacity' yake kununua 'lines' nyingi zaidi za dawa kuliko ilivyo sasa, ambapo MSD inaweza ku-supply only 65% ya mahitaji.
2. Bohari ijiendeshe kibiashara.
3. Tuweke 'color code' kwenye dawa zote za serikali kwenye bohari; mfano labda dawa za serikali ziwe na rangi ya 'pink' pekee, na rangi hii iambatane na 'bar code', na kuwe na 'task force' maalum ya ukaguzi wa pharmacy za binafsi na ikitokea dawa ya serikali ikakutwa kwenye pharmacy yoyote ile kuwe na adhabu kali.
4. Bohari ya Dawa (MSD), kwa makubaliano maalum na hospitali husika, iruhusiwe kufungua pharmacy zake kwenye hospitali zote nchini ili iuze moja kwa moja kwa wateja. Tunaweza kuanza na hospitali chache za mfano - kama Muhimbili, Amana, Mwananyamala, Temeke, Sekou Toure, Za Rufaa za Mikoa na baadhi ya Wilaya, Vituo Vya Afya na Zahanati; Ili kuliko wateja wa hospitali za serikali kwenda kununua dawa kwa bei ya kurusha kwenye pharmacy za watu binafsi kule nje wanunue kwa bei nafuu ya serikali ndani ya hospitali zetu.
5. Tuongeze kasi ya kusajili wananchi wote kwenye Mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote ili kuongeza financing kwenye mfumo wa afya wa serikali zaidi ya kutegemea bajeti tu.
6. MSD wakiishakuwa na pharmacy yao ndani ya health facility watakaa na wataalamu na menejimenti ya hospitali husika na kuorodhesha madawa wanayohitaji na MSD kuhakikisha yapo kwenye pharmacy yao kwenye kituo husika.
Mwisho.

No comments: