Na:George Binagi-GB Pazzo & Vesterjtz
Mbunge
Mteule wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
Stanslaus Shing’oma Mabula, amewahakikishia Machinga Jijini Mwanza kuwa
wataendelea kufanya biashara zao katika maeneo mbalimbali ya katikati ya Jiji
hilo kama...
yaliyotengwa na uongozi wa halmashauri.
yaliyotengwa na uongozi wa halmashauri.
Mabula aliyasema hayo jana wakati akiwashukuru
wakazi wa Jimbo hilo kwa kumchagua kuwa mbunge wao katika Mkutano wa hadhara
uliofanyika Uwanja wa Mbugani, kufuatia uvumi unaoezwa mitaani kwamba machinga
pamoja na mamantilie wataondolewa katikati ya Jiji la Mwanza kufuatia ushindi
wake.
“Mtu kaenda Makoroboi, Stand ya Tanganyika,
Sahara, Soko la Igoma pamoja na maeneo mengine na kuwaambia Machinga na
Mamantilie kuwa Mabula ameingia madarakani, cha moto mtakiona. Nataka msikilize
kauli yangu leo kwamba sikuja kuitengua torati, nitaendelea kushirikiana na
ninyi ili muwe bora, tena zaidi ya miaka mitano iliyopita”. Alisema Mabula.
Katika hatua nyingine Mabula amewashukuru wakazi
wa Jimbo la Nyamagana kwa kumuamini na kumchagua kuwa mbunge wao, kwani wakati
akiwa Mstahiki wa Jiji la Mwanza yeye
pamoja na wanaccm wenzake walisemewa mambo mengi mabaya ambayo kimsingi
hayakuwa na ukweli wowote.
“Wamama walinyanyasika sana, walitemewa mate, walichaniwa
nguo, walipondwa mawe, walitukanwa, walidharirishwa. Pia tulisemewa na
kushuhudiwa uongo kila kona. Ninyi wenyewe mnakumbuka tuliambiwa tumevunja
matorori, tumeiba maandazi , lakini nawashukuru maana wananchi wa Nyamagana
walisema huyo huyo alieiba maandazi, kumwaga mchele na kuvunja matorori ndie
atakuwa mtetezi wetu.
Nae Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatu,
aliwashukuru Watanzania wote kwa kukichagua chama hicho kuanzia ngazi ya
Madiwani, Wabunge pamoja na Rais ambapo Dkt.John Pombe Magufuli aliibuka na
ushindi wa asilimia 58.46
Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili
iliyopita ya Octoba 25 kote nchini, Mabula aliibuka mshindi katika Jimbo la
Nyamagana kwa kupata kura 81,017 na hivyo kumuondoa aliekuwa mbunge wa jimbo
hilo Ezekiel Wenje kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema aliepata
Kura 79,280.
No comments:
Post a Comment