Sunday, November 8, 2015

PAPAA WEMBA AFANYA MAAJABU KWENYE TAMASHA LA KARIBU MUSIC FESTIVALS 2015

DSC_1032
Mwanamuziki nguli wa dansi kutoka DRC Congo, Papaa Wemba kushoto akiimba na kucheza sambamba na madansa wake jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la muzuki la Karibu Music Festival msimu wa pili linaloendelea katika viwanja vya Mwanakalenge,mjini Bagamoyo. 
DSC_1025
Papaa Wemba akiimba jukwaani kwenye tamasha la Karibu Music Festival 2015, usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mwanakalenge, mjini Bagamoyo
DSC_1099
Papaa Wemba akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani ) kwenye tamasha la Karibu Music Festival 2015, usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mwanakalenge, mjini Bagamoyo

DSC_1027
Wanenguaji wa Papaa Wemba wakishambulia jukwaa kwa style ya aina yake ambao walikuwa kivutio katika tamasha hilo..
DSC_1083
Sebene likiendelea jukwaani..
DSC_1102
Host wa tamasha la Karibu Music Festival 2015, Mc Lulu akipata kuimbisha mashabiki waliofurika katika tamasha hilo kwa kuimba sambamba na Papaa Wemba (Hayupo pichani) kibao cha "Show Me the way"..
DSC_1087
Papaa Wemba katika ubora wake..
DSC_1130
DSC_1030
Dansa akifanya yake jukwaani..
DSC_1063
DSC_1080
Papaa Wemba..
DSC_1090
Mwenyekiti wa tamasha la Karibu Music Festival, Amarido Charles (kushoto) akiwa pamoja na mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Bodenim 'Bo' katika viunga vya tamasha hilo viwanja vya Mwanakalenge..

(Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Na Andrew Chale, Modewjiblog
[BAGAMOYO-TANZANIA] Mwanamuziki kutoka Congo mwenye makazi yake nchini Ufaransa, Papaa Wemba, ameweza kuonyesha ukomavu wake kwenye muziki wa dansi licha ya kuwa na uri wa miaka 66, kwa kupiga shoo ya aina yake usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Karibu Music Festival 2015 linaloendelea ndani ya viwanja vya Mwanakalenge, Bagamoyo-Tanzania.
Katika shoo hiyo, Papaa Wemba aliweza kupanda jukwaani akiwa na bendi yake na kupiga nyimbo zaidi ya tano zilizokonga nyoyo mashabiki lukuki waliofurika ndani ya viwanja hivyo vya Mwanakalenge mjini hapa.
Papaa Wemba ambaye anatamba kwa muda mrefu na wimbo wa “Show Me The Way” ameweza kuwa miongoni mwa wasanii wa muziki wa dansi kutoka DRC Congo kufika Tanzania kwa mara ya pili sasa kwa vipindi tofauti huku watanzania wengi wakionyesha kumkubali na kufuatilia muziki wake mara kwa mara.
Baada ya shoo hiyo Papaa Wemba aliwashukuru Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi na kumuunga mkono katika muziki wake ambapo alieleza kuwa tamasha hilo la Karibu Music Festival licha ya kuwa change kwa kufanyika mwaka wa pili, huko linakoelekea litakuwa kubwa zaidi na kuwa maarufu.
Katika shoo hiyo, Papaa Wemba aliimba nyimbo zaidi ya nne huku akiimba pia vibao kadhaa vilivyowahi kutamba miaka ya nyuma pamoja na nyimbo mbalimbali zikiwemo mpya.
Tamasha hilo ambalo leo Novemba 8.2015, linatarajiwa kufikia tamati, linaratibiwa na Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO) na Legendary Music Entertainment and Promotions Co. Ltd, T kwa kushirikiana na kampuni ya kinywaji cha Jebel Coconut. Wadhaminiwa wengine ni pamoja na Swiss Embassy, Precision Air, Coca Cola, Mwananchi Communication, Kaya fm, Magic fm, Focus Outdoor, Jovago, Kaymu na Time tickets.

No comments: