Tuesday, May 17, 2016

ipindi cha Jukwaa Langu May 16 2016. Ziara ya Waziri mkuu UK. Uraia pacha

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na waTanzania waliojumuika kumsikiliza jijini London

Kipindi cha JUKWAA LANGU hukujia kila Jumatatu kikiongozwa na Mubelwa Bandio toka Beltsville Maryland, USA, kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoihusu Tanzania ya sasa na ile tuitakayo.
Ni Tanzania kutoka jicho la DIASPORA
Na katika kipindi cha juma hili, tulizungumza na Chris Lukosi, ambaye alitupa muhtasari wa ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa huko nchini Uingereza.
Muhtasari huo ulizua na mjadala mkali juu ya ahadi za serikali kuhusu vibali maalum kwa waTanzania waishio nje ya nchi.
Karibu

No comments: