Sunday, December 18, 2016

KIOJA CHA MWAKA >>>>BWANAHARUSI AINGIA MITINI MUDA MCHACHE KABLA YA NDOA JIJINI MBEYA

Samwel Mwakalobo Bwanaharusi ambaye ameingia mitini muda mchache kabla kuingia kanisani kufunga ndoa  katika kanisa la K.K.K.T Isanga jijini Mbeya.



Na JamiiMojaBlog ,FahariNews
Mwisho wa mwaka 2016 huenda ukamaliza na kituko cha aina yake katika  Mitaa ya Isanga Jijini Mbeya Mkoa wa Mbeya  mara baada ya bwanaharusi kuingia mitini masaa machache kabla ya kufunga ndoa.
Tukio hilo la aina yake limeibua maswali mengi kwa ndugu jamaa na marafiki ambao walikuwa tayari kwa maandalizi ya kuhudhuria harusi hiyo kuanzia kanisani hadi ukumbini.
Imeelezwa kuwa mipango yote ya harusi ilifanyika kwa pande zote mbili kushiriki  kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa kufuatwa hadi hatua ya mwisho ya kuingia kanisani ambapo kama kawaida ndugu jamaa wote walihudhuria kanisani kwa lengo la kushuhudia  tukio hilo .
Tukio rasmi lilianza majira ya saa 7 mchana katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa   Isanga jijini Mbeya Desemba 16   ambapo kama kawaida Bibi harusi akiongozana na wapambe wake akifuata na msafara wa magari zaidi ya manne akitokea Saloon  na kuingia kanisani hapo.
Baada ya bibi harusi kuingia kanisani tayari kwa kufunga ndoa hiyo  taarifa zilianza kuenea kuwa bwanaharusi hayupo kanisani hapo na hajulikani mahali alipo.
Kadri muda ulivyozidi kwenda bila bwana harusi kufika kanisani hapo baadhi ya Ndugu, jamaa  na watu waliohudhuria harusi hiyo walianza kuhoji ambapo kwa muda huo yalipita zaidi ya masaa 4 bila chochote kuendelea kanisani hapo.

Kadi ya mualiko kwa ajiliya sherehe

Bibi harusi Given Mgaya Mkazi wa Isanga jijini Mbeya   

No comments: