Monday, December 12, 2016

WAHITIMU ZAIDI YA 2000 CHUO KIKUU SAUT JIJINI MWANZA KUTUNUKIWA VYETI MBALIMBALI WIKENDI HII

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustin SAUT, Padri, Dkt.Thadeus Mkamwa (kushoto), akitoa taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho yatakayofanyika kwa siku mbili, Ijumaa Disemba 16 na Jumamosi Disemba 17 mwaka huu chuoni hapo Malimbe Jijini Mwanza. 

Kulia ni Bernald James ambaye ni Mkuu wa Mawasiliano, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mwanza Mhashamu Yuda Thadeus Rwaichi.

Wahitimu 2421 wa fani mbalimbali wanatarajiwa kutunukiwa vyeti, shahada, shahada za uzamili na uzamivu katika mahafali hayo huku wanafunzi wanafunzi 746 wakishindwa kutunukiwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutolipia ada.

Mahafali hayo yatatanguliwa na Siku ya Jamii itakayofanyika Jumatano Disemba 14 ambapo kutakuwa na Maonesho ya Kitaaluma.
BMGHabari</ div>
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustin SAUT, Padri, Dkt.Thadeus Mkamwa (kushoto), akitoa taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho yatakayofanyika kwa siku mbili, Ijumaa Disemba 16 na Jumamosi Disemba 17 mwaka huu chuoni hapo Malimbe Jijini Mwanza. 
Bernald James ambaye ni Mkuu wa Mawasiliano, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.
Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa
kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho yatakayofanyika kwa siku mbili, Ijumaa Disemba 16 na Jumamosi Disemba 17 mwaka huu chuoni hapo Malimbe Jijini Mwanza. 
Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho
Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho
Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT 
Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho
Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho
Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho
Wanahabari na wajumbe wa baraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho
Wahitimu 2421 wa fani mbalimbali wanatarajiwa kutunukiwa vyeti, shahada, shahada za uzamili na uzamivu katika mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine SAUT cha Jijini Mwanza.

Makamu Mkuu wa chuo hicho Dkt.Thadeus Mkamwa amesema wahitimu hao wakiwemo watatu wa shahada za uzamivu watatunukiwa shahada zao kwenye Mahafali yatakayofanyika ijumaa na jumamosi wiki hii chuoni hapo.

Amesema mahafali hayo ambayo mgeni rasmi atakuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mwanza Mhashamu Yuda Thadeus Rwaichi yatatanguliwa na Siku ya Maonesho Kitaaluma yatakayohusisha wanafunzi na wahadhiri kutoka kila kitivo na idara.

Hata hivyo Dkt.Mkamwa amesema wanafunzi 746 wameshindwa kuhitimu masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kulipa ada.

No comments: