Wednesday, June 14, 2017

MIL 85,000,000 ZAPATIKANA ZITAJENGA MADARASA MATANO SHULE YA MSINGI HONDOGO

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo June 14, 2017 Ameeleza dhamira yake kuhusu ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika shule ya Msingi Hondogo iliyopo katika Kata ya Kibamba.

MD Kayombo ametoa ufafanuzi huo ofisini kwake alipokuwa akitoa tathmini ya ziara yake aliyoifanya katika Shule ya Msingi Hondogo Jana tarehe 13 June 2017.


Katika ziara hiyo ambayo Mkurugenzi aliambatana na Mchumi Mkuu wa Manispaa, na Ofisa Elimu Msingi walikagua maeneo yote ya shule hiyo ikiwemo majengo na kubaini kuwa Kuna baadhi ya majengo ambayo yapo katika hali ya uchakavu hivyo kuamua kujenga madarasa mapya matano ili kuwaimarishia wanafunzi kuwa na mazingira rafiki ya kusomea.

Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa ujenzi huo utakaoanza hivi karibuni wa vyumba vitano vya madarasa unaakisi pia ujenzi wa vyumba vya madarasa nane na matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza, vivyo hivyo katika Shule ya Msingi Kawawa na Shule ya Sekondari Mburahati ambapo kote huko ameelekeza kuanza haraka ujenzi wa Madarasa sambamba na Vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu.

Mkurugenzi Kayombo ameishukuru Bank ya CRDB kwa kuchangia shilingi Milioni 68,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo ambapo ameeleza kuwa Ofisi yake imetoa jumla ya shilingi milioni 17,000,000.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

No comments: