Sunday, October 15, 2017

BONANZA LA MICHEZO JIJINI TANGA LAHUDHURIWA NA MAMIA YA WAKAZI WA JIJI HILO


Wapenzi wa mchezo wa mpira wa kikapu wakishuhudia baadhi ya timu zilizoshiriki bonanza hilo zikichuana leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga ambalo lilikuwa na msisimuko mkubwa likiwakutanisha mamia ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga
TIMU za mpira wa Pete (netball) za Bandari na Jiji zikichuano katika bonanza hilo ambapo kwenye mchezo huo,Jiji iliweza kuibuka na ushindi wa  mabao 30-1 dhidi ya
wapinzania wao ambapo kipindi cha kwanza Jiji iliweza kuongoza kwa mabao 18-0 dhidi ya Bandari
Wachezajji wakichuana katika mechi ya mpira wa pete kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga leo katika bonanza la michezo ambalo limeandaliwa na Radio ya TK FM kwa kudhaminiwa na Tanga City Lounge,Tanga Fresh,Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF),Vodacom,Amic Design,Chuo cha Utumishi wa Umma(TPSC) Tawi la Tanga,Katani Limited,Leen Events Planner,Shirika la Maendeleo la BRAC Tanzania,Jaysen Studio 
Wananchi wa mkoa wa Tanga wakishuhudia uhondo wa michezo mbalimbali katika bonanza hilo
Wachezaji wa timu ya mpira wa pete ya chuo cha Utumishi Mkoani Tanga wakitoka uwanjani mara baada ya mechi yao kumalizika
Wachezaji wa timu ya Maveterani ya Tanga Middle Age wakipasha kabla ya kuwavaa wapinzani wao Kilombero Veterani ambapo Tanga Middle Age walishinda kwa bao 1-0

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Tanga aliyetembelea banda lao waliloweka kwenye bonanza hilo kwa lengo la kuhamasisha jamii kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na matibabu


Wachezaji wa timu za maveterani wakichuana katika Bonanza hilo ambalo lilikuwa la aina yake kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Mjini Tanga ambalo liliandaliwa na kituo cha Radio cha Jijini Tanga (TK)

Mashabiki wa michezo wakifuatilia kwa umakini bonanza hilo
Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Denis Kapinga akitolea ufafanuzi baadhi ya huduma wanazozitoa wakati wa bonanza hilo

Msimamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga,Dinna Mlwilo kushoto akisisitiza jambo kwa wananchi waliofika kwenye banda lao leo kwenye bonanza la Michezo ambalo lilifanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga
Wafanyakazi wa Radio TK FM ya Jijini Tanga kushoto ni Mamy Mohamed ambaye ni Meneja wa Kituo hicho kulia ni George Kivumbi ambaye ni Program Manager katikati ni DJ Rogger Kiss wakiwa katika bonanza hilo
 Mamy Mohamed ambaye ni Meneja wa Kituo cha Radio cha TK FM ya Jijini Tanga akitoa utaratibu wa zawadi kwa washindi mara baada ya kumalizika bonanza hilo
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi Robert Gabriel akiwa na Mkurugenzi wa Radio TK ya Jijini Tanga,Saidi Othumani kushoto wakati alipokwenda kumwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella katika Bonanza hilo
 Mkurugenzi wa Radio TK ya Jijini Tanga,Saidi Othumani kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel
 Ally Choki mzee wa Farasi kulia akiwa na Luiza Mbutu kwenye jukwaa wakitumbuiza katika Bonanza la Michezo ambao liliandaliwa na Radio TK FM ya Jijini Tanga
 Wasanii wanaounda Bendi ya Twanga Pepeta wakitumbuiza Jukwaani
 Wasanii wanaounda Bendi ya Twanga Pepeta wakitumbuiza Jukwaani
 Baadhi ya washiriki  waliojitokeza katika bonanza hilo wakipiga picha ya pamoja
  Baadhi ya washiriki  waliojitokeza katika bonanza hilo wakipiga picha ya pamoja
Wananchi wakifuatilia Bonanza hilo

No comments: