Mgeni rasmi ambaye ni afisa elimu manispaa ya Iringa MWL .Tupe Kayinga akizungumza na walimu wanawake waliojitokeza kuelekea mkutano mkuu wa chama cha walimu manispaa ya Iringa.
katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale akizungumza na walimu wanawake waliojitokeza
kuelekea mkutano mkuu wa chama cha walimu manispaa ya Iringa.
Baadhi ya walimu wanawake waliohudhuria mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Walimu wanawake manispaa ya
Iringa walalamikia kutokuwepo kwa uwiano wa viongozi wanawake na wanaume katika
sekta nyeti kama vile wakuu wa shule,maafisa elimu kata na wilaya wakati walimu
wa wanawake ndio wengi hivyo inafifisha ndoto za kuwa viongozi kwa kuwa
wanauwezo wa kuongoza na kusimamia mambo mengi yakaenda kama yalivyopangwa.
Hayo yamesemwa na walimu
wanawake katika mkutano mkuu wa chama cha walimu wanawake kilichokuwa
kinaongozwa na katibu wa wilaya mwl. Fortunata Njalale katika ukumbi wa chuo
kikuu huria tawi la Iringa.
Akisoma risala iliyoandaliwa
na kamati ya kitengo cha walimu wanawake MWL. Evon Mhewa alisema kuwa walimu
wanawake wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi katika kukamilisha majukumu
yao.
“Mwalimu wa kike anacheleweshewa
kulipwa madeni mbalimbali anayokuwa anaidai serikali maana bila kulipwa madeni
yetu walimu hawawezi kufundisha kwa moyo kwa kuwa maisha yanakuwa magumu na
kuwapelekea kubuni njia mbadala za kujiingizia kipato” alisema Mhewa
Mhewa alizitaja changamoto
nyingine ni kutopata nyongeza ya mishahara ya kila mwaka na kusimama kwa mwaka
wa pili sasa,walimu kutopandishwa madaraja na wengine kupandishwa na kupokwa
mshahara pamoja na walimu wanawake kutokuwa na uwiano wa vyote katika sekta
nyeti.
“Sisi walimu wa kike kwa
sasa tumesoma sana na tunaweza kuwa viongozi sehemu yoyote kwa kuwa tayari
tumethibisha hilo kwa wanawake waliopewa kazi hiyo kwani wameifanya ipavyo na
kuleta matokeo chanya kwa serikali hivyo tunaomba walimu wanawake tupewa nafasi
katika ngazi ambazo tunastahili” alisema Mhewa.
Akijibu risala hiyo mgeni
rasmi ambaye ni afisa elimu manispaa ya Iringa MWL .Tupe Kayinga alisema kuwa
ni kweli walimu wanamadi mengi serikalini lakini akasema kuwa hiyo yote
imetokana na swala la uhakiki wa watumishi hivyo mchakato wa uhakiki
ukimalizika kila kitu kitakuwa sawa ninauhakika na hilo.
“Unajua serikali
imechelewesha maswala mbalimbali ambayo ni kero kwa walimu kutokana na uhakiki
hivyo nawaomba walimu wawe na uvumilivu kwa kuwa kila kitu kitakuja kutengemaa
kama ilivyokuwa hapo awali” alisema Kayinga
Kayinga aliwataka walimu
wanawake kuendelea kusoma ili kuwa na elimu ndio itakayowapa nafasi mbalimbali
ambazo zinashikiriwa na walimu wanaume hivyo bila kuwa na elimu walimu wanawake
wataendelea kuongozwa na walimu wanaume kila sekta.
“Najua kuwa walimu wanawake
wanakipawa cha kuwa viongozi lakini mitaala mingi inataka walimu kuwa na elimu
ili kupata kuongoza sekta mbalimbali sasa inatubidi walimu kujiendeleza
kimasomo ili kukidhivigezo ambavyo mara nyingi imekuwa ni elimu ya walimu
anayepaswa kupewa kitendo husika” alisema Kayinga
Aidha Kainga aliwataka
walimu wanawake kugombea nafasi mbalimbali zinazojitokeza ili kupata nafasi za
kuongoza na sio kila wakati kuwaacha walimu wanaume wakigombea pekee yao.
“Tumieni fursa za kugombea
nafasi zinazojitokeza msiogope wanawake mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kuogmbea
kwa kuwa katika kada ya ualimu walimu wanawake tupo wengi hivyo kuanzia saizi
walimu wanawake amkeni mjitume kuhakikisha mnagombea” alisema Kayinga
Naye katibu wa chama cha
walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale alisema kuwa mkutano huo ni wa
kikatiba kwa mjibu wa katiba ya chama cha walimu taifa hivyo katiba imewaagiza
kukaa na viongozi wa walimu wanawake kuzijadili changamoto za wanawake ili
kuzipeleka katika mkutano mkuu wa wilaya.
“Leo tupo walimu wanawake
pekee yetu ili kubaini changamoto zetu na kuzipeleka kwenye mkutano mkuu na
kuweza kuzitetea kwa pamoja ili kuboresha maslai ya walimu wanawake ambao
wamekuwa wanakumbana na changamoto nyingi sana wawapo kazini” alisema Njalale
Njalale alisema kuwa walimu
wanawake wamekuwa na mwamko wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuwa
wanauwezo wa kuwa viongozi na kuongoza kwa kupata matokeo chanya.
“Tunakitengo cha walimu
wanawake taifa kimetusaidia sana walimu wanawake kupata ujalisi na kuacha uoga
kugombea nafasi mbalimbali hivyo kwa sasa walimu wakiume wajipange sana maana
walimu wanawake tumedhamilia kugombea nafasi yeyeto itakayojitokeza katika
chama chetu cha walimu” alisema Njalale
Njalale aliwapongeza walimu
wanawake wanaothubutu kugombea nafasi mbalimbali kwa kuwa wamekuwa wakishinda
na wanafanya kazi ipasavyo na kusema kuwa walimu wanawake wanaweza bila
kuwezeshwa.
No comments:
Post a Comment