Wednesday, December 13, 2017

KUMBE UNGA WA MUHOGO HUTENGENEZEA KIWASHIO MOTO CHA KIBIRITI?!


Uongozi wa Mkikita ukiwa na uongozi wa kiwanda cha Unga cha Ukaya, Mkuranga, Pwani, ulipotembelea kiwanda hicho ambacho wako mbioni kuingia mkataba wa kusaga mihogo ya wanachama
wao kupata unga wa kuuza katika masoko ya ndani na nje ya nchi.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui S. Kissui, Mkurugenzi wa Kiwanda, Ibrahim, Meneja wa Kiwanda, Matanga na Mkurugenzi wa Mkikita, Adam Ngamange.




Na Richard Mwaikenda, Mkuranga

UNGA wa muhogo unatumika kutengenezea kishungi cha kuwashia moto katika vibiriti.

Jambo hilo lilithibitishwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kusaga muhogo cha Ukaya, Mkuranga, Ibrahim mbele ya uongozi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) uliotembelea kiwanda hicho.

Alisema kuwa miongoni mwa wateja wakubwa wa unga wao ni Kiwanda cha kutengenezea vibiriti cha Kasuku kinachoutumia kwa kutengenezea kishungi cheusi cha njiti ya kibiriti kinachotumika kuwasha moto.

Uongozi wa Mkikita ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Kissui S. Kissui na Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao huo, Adam Ngamange ulitembelea kiwanda hicho kwa lengo la kuingia nao mkataba wa makubaliano ya kukitumia kusaga mihogo ya wanachama wao kupata unga utakaouzwa na katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Ibrahim alisema unga pia hutumika kutengenezea dawa ya kuzuia kuhara, pombe, mafuta, chakula cha wanyama na binadamu.



Imeandaliwa na Richard Mwaikenda;Kamanda wa Matukio Blog 0715-264202

No comments: