Monday, December 18, 2017

SAFARI YA WAZALENDO 47 ILIVYOINGIA SIKU YA PILI WAKATI WAKIELEKEA KILELE CHA UHURU,KATIKA MLIMA KILIMANJARO

Baada ya kupumzika katika kituo cha Mandara katika siku ya kwanza ,Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Jenerali George Waitara aliongoza Wazalendo 47 kutoka jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),Wanahabari,Marafiki wa China na Tanzania pamoja na watumishi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika siku ya pili ya kuelekea kilele cha Uhuru kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru wa Tanzania.
Miongoni mwao alikuwepo ,Balozi Mstaafu na Mwenyekiti
Mstaafu wa Bodi ya Utalii ,Tanzania ,Charles Sanga.
Safari ya kuelekea kituo cha pili cha mapumziko cha Horombo ili chagizwa na nyimbo mbalimbali ambazo ziliongeza morali kwa wapandaji.
Makao makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) yaliwakilishwa vyema na Meneja wake wa Mawasiliano ,Pascal Shelutete .
Mwanahabri Vicky Kimaro aliwakilisha pia Magazeti ya serikali ya HABARI LEO.
Mwanahabari George Mbara alikiwalisha vyema kituo cha luniknga cha ITV.
Mwanahabari Jamila Omar yeye alifanya uwakilishi wa kituo cha Luninga cha Channel ten.
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) liliwakilishwa na Bertha Mwambela 
Na Safari iliendelea ikiongozwa na Slogan ya "Mdogo Mdogo"
Mapumziko yalikuwepo mara baada ya kutembea sehemu yenye umbali mrefu.
Wengine walitumia mapumziko hayo kwa ajili ya kupata picha za kumbukumbu ya pamoja.
Na baadae Safari iliendelea.
Hali ya hewa katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro haitabiliki ghafla linaweza onekana jua na muda mchache tu mvua ikanyesha ,hivyo wapandaji hua wamejiandaa na aina yoyote ile ya hali kama inavyoonekana hapa wakiwa katika mavazi rasmi ya kuzuia mvua pindi walipowasili eneo la Nusu njia kwa ajili ya kupata chakula.
Wazalendo wakatumia mapumziko ya Nusu njia kupata chakula cha mchana.
Safari ikaendelea kwa kupita katika mito mbalimbali ambayo imekuwa ikitiririsha maji kwa wingi.
Wazalendo walipita katika madaraja mbalimbali wakati wa upandaji wa mlima huo.
Wenye kuhitaji msaada walipata kwa wakati.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibook alihakikisha anaongozana na Wazalendo hao katika safari ya kuelekea kilele cha Uhuru akiwa ndiye mwenyeji wa ugeni huo.
Hatimaye safari iliyoanza saa 2:30 za asubuhi katika kituo cha mapumziko cha Mandara ikahitimishwa majira ya saa 11:00 za jioni katika kituo cha mapumziko cha Horombo kwa ajili ya kujiandaa na safari ya kuelekea kituo cha Kibo kabla ya kuelekea kilele cha Uhuru.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini aliyekuwa katika msafara wa Wazalendo hao.

No comments: