Tuesday, February 20, 2018

MBUNGE MGIMWA AMETOA BATI 590 NA MIFUKO YA SARUJI 220 KWA AJILI YA UJENZI NA UKARABATI WA MADARASA KATA YA IHALIMBA

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na walimu juu ya mambo aliyoyafanya kwenye kata hiyo kielimu ambapo ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi  na ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya Ihalimba
 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa na viongozi wa elimu ngazi ya wilaya kata na vijiji wakati wa mkutano baina ya viongozi hao na walimu wa shule za kata ya Ihalimba
 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akimkabidhi zawadi mmoja ya mwalimu aliyefanya vizuri darasani kwa kuongeza ufaulu

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wanaofundisha katika kata ya Ihalimba katika jimbo la
Mufindi Kaskazini 


 Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.

 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi  na ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya Ihalimba huku lengo likiwa kuboresha sekta ya elimu na afya kwa wananchi.

Akizungumza na walimu wa kata hiyo mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmuod Mgimwa alisema kuwa ameamua kuwekeza katika elimu na afya kwasababu wananchi wakifanikiwa kupata vitu hivyo viwili kwa wakati watafanya maendeleo kwa kasi kubwa kulingana na wakati uliopo na kuendana na mazingira wanayoishi.

“Hivi ndio vipaumbele vyangu kwa kijiji hiki kwa wakati huu maana nimegundua kuwa changamoto kubwa ni kuwa shule nyingi za msingi zilijengwa miaka mingi iliyopita sasa zimechakaa na sio rafiki kwa wanafunzi kuwasaidia kupata elimu bora hivyo nimeanza na hilo pamoja na kuchangia maendeleo kwa kuboresha sekta ya afya ili wananchi wakiugua waweze kutibia hapa hapa kijiji kwa kuwa nina uhakika huduma itakuwa inatolewa kwa ustadi mkubwa na yenye ubora unaotakiwa” alisema Mgimwa

Mgimwa alieleza maeneo ambayo ametoa bati na mifuko ya saruji kuwa ni shule ya msingi Nundwe Bati 160 kwaajili ya nyumba ya walimu 60 na ukarabati wa paa la madarasa, bati 100. shule ya msingi Vikula bati 100 na saruji 50, shule ya msingi Mong'a bati 50,Zahanati ya Ugesa bati 30 na saruji 40 kwaajili ya nyumba ya mganga wa kijiji cha Wami, ujenzi wa nyumba ya mganga wa kijiji cha Mbalwe bati 100 na saruji 20,Ihalimba sekondari nyumba ya mganga bati 50 na fedha tshs 1,100,000 kwaajili ya dari jengo la maabara na kununua pampu ya maji.

“Hizi ni gharama ni kata moja tu ya Ihalimba ambazo nimezitafuta nako kujua mimi hivyo lazima walimu mjue kuwa kuwa mbunge ni kazi kubwa sana na lengo la kuwa mbunge nikuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo ambayo yanatakiwa kwa wakati sahihi hivyo napenda kuwapa habari vijiji na vitongoji vingine kwenye jimbo langu kuiga mfano wa kata ya Ihalimba kwa kujituma kuleta maendeleo” alisema Mgimwa

Mgimwa alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuendelea kumuunga mkono katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo kwa kuwa wanajinea kazi anayoifanyia hivyo wasikubali kulishwa maneno na watu wasiopenda maendeleo.

Aidha Mgimwa aliwataka walimu kumwambia changamoto ambazo wanakumbana nazo ili kuzitatua na kuhakikisha walimu wanafundisha katika mazingira mazuri.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ihalimba wilayani Mufindi mkoani Iringa Award Mahanga  amempongeza mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Mahmoud Mgimwa kwa kuendelea kutatua changamoto zinazoikabiri sekta ya elimu kwa kuchangia saruji mifuko 200 na bati 590 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya shule za msingi na sekondari za kata hiyo.
Mahanga aliesema kuwa mbunge Mgimwa amekuwa akijitoa kwa kutatua changamoto za wananchi kwa ajili ya maendeleo ya eneo husika.
Aidha Mahanga alisema kuwa mbunge huyo amechangia kwenye sekta ya afya ambapo amefanikisha ujenzi wa zahanati kwenye kila kijiji cha kata hii ya Ihalimba

Lakini pia Mahanga alimshukuru mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kwa jitihada zake za kuleta maendeleo kwa kushirikiana na wananchi na kuahidi kuwa watandelea kuzitangaza kazi anazozifanya ili wananchi wote wajue anafanya kazi gani na kupunguza maneno ambayo yamekuwa yakisemwa bila kuwa na ushaidi juu ya utendaji wa mbunge huyo.

“Kweli kabisa mbunge wetu amekuwa akifanya kazi kubwa sana ila sisi tumekuwa hatuzisemi kazi za mbunge kwa wananchi hivyo kuchochea chuku baina ya wananchi na mbunge hivyo kuanzia leo nitakuwa ninazisemea kazi za mbunge kila kwenye mkutano wa kijiji” alisema Mahanga

No comments: