Tuesday, February 20, 2018

MHE BITEKO AANZA ZIARA MKOANI MBEYA AMPA HEKO RC MAKALLA USIMAMIZI WA SEKTA YA MADINI

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla wakati alipozuru ofisini kwake mara baada ya kuwasilia mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku, Leo 20 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-WazoHuru Blog
Picha ya pamoja Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (katikati) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla
  mara baada ya mazungumzo wakati alipozuru ofisini kwake akiwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, Leo 20 Februari 2018. Wengine pichani ni Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njenza CCM (Kulia), Katibu tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi Mariamu Mtunguja (Wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika (Wa kwanza kushoto).

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akisikiliza kwa makini taafifa kuhusu sekta ya madini kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla wakati alipozuru ofisini kwake mara baada ya kuwasilia mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku, Leo 20 Februari 2018.

Na Mathias Canal, Mbeya

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea kiwanda cha kutengeneza Samani mbalimbali zinazotokana na Marble, kukagua shughuli za uchakataji Madini ya malumalu na mradi wa Pandahili (Niobiaum).

Maeneo mengine atakayotembelea ni pamoja na mgodi wa Sunshine uliopo katika Wilaya ya Chunya ambapo atazungumza pia na wachimbaji wadogo katika migodi atakayotembelea.

Mara baada ya kuwasili katika Mkoa wa Mbeya Mhe Biteko amesifu juhudi za Mkuu wa Mkoa huo Mhe Amos Makalla kwa uthubutu mkubwa katika utendaji ikiwa ni pamoja na usimamizi madhubuti katika sekta ya Madini.

Pamoja na pongezi hizo Mhe Biteko amemsihi Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya kuongeza juhudi zaidi ili kutimiza ndoto ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kuwatumikia watanzania na kupelekea kunufaika na rasilimali zao ikiwemo sekta ya Madini.

Alisema kuwa Sekta ya Madini bado ni muhimu hivyo inahitaji kulelewa ili ikuwe na hatimaye kuongeza ufanisi katika uchangiaji wa pato la Taifa 

Alisema kila kiongozi ana wajibu mkubwa kuwa mbunifu katika uwajibikaji wake huku akiongeza kuwa Jukumu la msingi la kiongozi ni pamoja na kutafsiri ndoto za Rais Magufuli ili kuwafanya wananchi kunufaika na uongozi bora na utendaji wa serikali ya awamu ya tano.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makala amesisitiza kuendeleza ushirikiano madhubuti na Wizara ya Madini ili wananchi Mkoani humo wanufaike na matunda ya kukichagua Chama Cha Mapinduzi kuongoza dola.

MWISHO.

No comments: