Thursday, March 8, 2018

SERIKALI YAFUNGA KIWANDA KWA SIKU 14

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, akizungumza na
wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza nywele cha SH. Afrique Tanzania Limited leo Machi 7, 2018, wakati wa ziara yake ya kushtukiza kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi ipasavyo Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini, ikiwa ni pamoja na wale ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

SERIKALI imesitisha shughuli za uzalishaji kwenye kiwanda cha kutengeneza mifuko ya nailoni (viroba), cha TASIPA kilichoko jijini Dar es Salaam kwa siku 14 kuanzia leo Machi 7, 2018 baada ya kubainika kuwa kiwanda hicho kinahatarisha maisha ya wafanyakazi wake.

Sambamba na hilo, kiwanda hicho pia kimetozwa faini ya shilingi milioni 18 kwa kukiuka sheria ya usalama na afya mahala pa kazi.

Aidha Mhe. Mavunde pia amevitoza faini ya jumla ya shilingi milioni 22.8 viwanda vya Hengji Investment, ambacho pia kinatengeenza viroba (mifuko ya nailoni), na kiwanda kingine cha kutengeneneza nywele cha SH. Afrique Tanzania Limited kwa makosa mbalimbali ya kukiuka Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini.

“Katika kukagua Sheria za usalama na afya mahala pa kazi, tumebaini kuwa mazingira ya kiwanda hiki cha TASIPA ni hatarishi mno kwa mfanyakazi kufanya kazi na tayari watu wa OSHA walikwishafika hapa na kutoa maelekezo, lakini hakuna kilichofanyika.” Alisema Mhe. Mavunde.

Naibu Waziri pia aliagiza kuwa muajiri huyo kutoa mikataba ya kazi kwa wafanyakazi wote kwa mujibu wa sheria namba 6 ya mwaka 2004 na mikataba iwe imekamilika n dani ya siku 14 na kuwasilishwa kwa Kamishna wa Kazi ili aipitie.

Awali Mheshimiwa Mavunde alitembelea kiwanda  cha kutrengeenza nywele na kupokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mikataba ya kazi, kufanya kazi kwa muda mrefu bila kulipwa malipo ya muda wa ziada na kufanya kazi kwenye mazingira ambayo yanahatarisha afya za wafanyakazi.

Kiwanda hicho kilitozwa faini ya shilingi milioni 8 na kutakiwa kurekebisha kasoro zote zilkizojitokeza ndani ya kipindi kifupi.

Naibu Waziri pia alikitoza faini kiwanda cha Hengji Investment Limited kinachojishughulisha na utengenezaji mifuko ya viroba kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria za kazi na usalama mahala pa kazi.

Ziara ya Naibu Waziri ambayo imeianza wiki iliyopita jijini Mwanza, inalenga kufuatilia maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziriu Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama aliyoyatoa Mwishoni mwa mwaka jana, kuwataka waajiri wote ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF), watekeleze wajibu huo wa kisheria vinginevyo wafikishwe mahakamani.

Tayari waajiri kadhaa wameanza kufikishwa mahakamani kwa kosa hilo na operesheni hiyo kwa mujibu wa Naibu Waziri ni endelevu na itafanyika nchi nzima.

 Kwa mujibu wa sharia ya usalama mahala pa kazi mfanyakazi huyu alipaswa kuvaa mask na gloves. hapa ni kiwanda cha TASUPA kinachotengeneza mifuko ya nailoni (viroba)
 Naibu Waziri Mvunde akishuhudia ukiukwaji wa sharia ya usalama mahala pa kazi kiwanda cha TASUPA
 Naibu Waziri Mvunde, (wapili kushoto), akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo, akizungumza na nmfanyakazi wa TASUPA ambaye alimkuta akifanya kazi ya kutengeneza mitambo ya kuchanganya masalia ya mifuko ya plastiki kiwanda cha TASUPA huku akiwa hana vifaa vya kujihami(protective gears).
 Naibu Waziri Mvunde, (wapili kushoto), akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo, akizungumza na nmfanyakazi wa TASUPA ambaye alimkuta akifanya kazi ya kutengeneza mitambo ya kuchanganya masalia ya mifuko ya plastiki kiwanda cha TASUPA huku akiwa hana vifaa vya kujihami(protective gears).
 Wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza nywele cha SH Afrique Tanzania Limited, wakimsikiliza Naibu Waziri Mabunde(hayupo pichani) alipozunhgumza nao.
 Naibu Waziri Mvunde, alipotembelea kiwanda cha SH Afrique
 Kamishna wa Kazi, Bi.Hilda Kabisa, (kushoto) akizunhguzma jambo.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, 9WCF), Bi. Rehema Kabongo.
 Msaidizi wa Meneja Mwajiri kiwanda cha kutengeneza nywele cha SH. Afrique Tanzania Limited, Bi.Domina Domisium, (kulia), akitoa maelezo ya uendeshaji wa kiwanda hicho, mbele ya Naibu Waziri Mhe. Mavunde
 Bi. Kabisa akimuhoji Bi.Domina
 Naibu Waziri Mvunde, akifurahia jambo na Meneja Uendeshaji kiwanda cha SH. Afrique Tanzania Limited, Bi.Kim Minju, (kulia). Katikati ni Bi. Rehema Kabongo.
 Mhe. Mavunde akizungumza na wafanyakazi wa SH. Afrique Tanzania Limited.
 Wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza mifuko ya nailoni (viroba) cha TASUPA.
 Naibu Waziri akitoa maagizo kiwanda cha TASUPA.
Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha TASUPA, kwa niaba ya wenzake akizungumza mbele ya Naibu Waziri, ambapo alieleza ukiukwaji mkubwa wa haki za wafanyakazi kiwandani hapo.

No comments: