Monday, May 28, 2018

VIJANA WASHAURIWA KUWA WASHIRIKI WA MAENDELEO SIO WANAOSUBIRI

 Rais wa AIESEC Tanzania, Amani Shayo akizungumza kuhusu AIESEC na kazi zake ambapo alisema jukwaa hilo lengo lake ni kuwasaidia vijana kujitambua katika masuala ya uongozi, anaamini kwamba jukwaa ni sehemu kubwa ya kufanikisha vijana kujitambua na kujiipanga kushiriki maisha yanayotakiwa katika jamii wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
 Mgeni rasmi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na vijana wa kutoka vyuo mbalimbali walioshiriki kwenye jukwaa la vijana la

KINANA, MBUYU KWENYE MSITU WA SIASA

Image may contain: 2 people, people smiling, people standing

Na Emmanuel J. Shilatu

Kanali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Abdulrahman Omar Kinana anatajwa kuwa katika orodha ya safu za viongozi mibuyu na migude kwenye misitu minene ya siasa yenye kuhimili tufani za kila aina pia Mwanasiasa anayependa kuheshimu utamaduni, utaratibu na mwenye kuishi kwa misingi ya nidhamu .

JUMIA FOOD YASHIRIKIANA NA WATEJA KUSAIDIA WATOTO




Na Jumia Food Tanzania

Katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Jumia Food kwa kushirikiana na wateja wake inaendesha kampeni ya kusaidia kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kampuni hiyo inayojihusisha na huduma ya chakula kutoka migahawa mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao, imeona ni vema kuwashirikisha wateja wake kwani wao ndio wadau wake wakubwa.

Kampeni hiyo inayokwenda kwa jina la ‘STANDY BY ME,’ kwa kiasi kikubwa inawategemea wateja kwa sababu kwa kila huduma ya chakula watayoifanya kupitia mtandao wa Jumia Food itakwenda moja kwa moja kumsaidia mtoto mmoja kituoni hapo.


Akifafanua namna wateja wanavyoweza kuchangia, Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Food

Water Mission Tanzania yazindua mradi wa maji wilayani Mwanga

Mkuu wa wilaya ya Mwanga, Bw. Aron Mbogho akikata utepe kuzindua mradi.
Mmoja wa wakazi wa kata ya Kiruru akitwishwa ndoo ya maji aliyochota kwenye mradi.

Thursday, May 24, 2018

Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza kuendelea kuboresha uhusiano wa kibiashara

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (kushoto) akizungumza na baadhi ya maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini, juu ya kuangalia njia bora za kudumisha uhusiano baina ya Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza nchini, katika Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es salaam, Mei 23, 2018. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa. 

LEO NI SIKU YA TATU YA KAMPUNI YA ASAS DAIRIES KUGAWA MAZIWA KWA WANAFUNZI IRINGA

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


Leo ni siku ya tatu kwa kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Ltd toka imetenga pakiti 120,000 za maziwa yenye thamani ya Sh Milioni 60 zilizoanza kugaiwa bure kwa wanafunzi zaidi ya 30,000 wa shule za msingi za serikali na binafsi za mjini Iringa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yake ya wiki ya maziwa.

Tuesday, May 22, 2018

BANK OF AFRICA ORGANISES AN IFTAR DINNER FOR CUSTOMERS IN DAR ES SALAAM

The Deputy Managing Director of BANK OF AFRICA – TANZANIA, Mr. Wasia Mushi delivers his welcoming remarks at the bank’s IFTAR Dinner at the Serena Hotel in Dar es salaam.

The Deputy Managing Director of BANK OF AFRICA – TANZANIA, Mr. Wasia Mushi in a jovial moment as he welcomes some of the esteemed clients of the bank who

WABUNGE WA MIKOA YA KUSINI WAIMWAGIA SIFA SERIKALI NA TANESCO KWA KUMALIZA KERO YA UMEME MTWARA NA LINDI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(kushoto), akifurahia jambo na Wazitri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, (watatu kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua,

Monday, May 21, 2018

RITTA KABATI CHALLENGE CUP MSIMU 2018 WAFUNGULIWA RASMI,TIMU ZAOMBWA KUCHUA FOMU KUSHIRIKI


 kulia ni Mwenyekiti wa mashindano ya Ritta Kabati challenge cup 2018 na kushoto ni katibu wa kamati ya mshindano hayo walipokuwa wakiongea na vyombo  vya habari kwenye ofisi zao zilizopo manispaa ya Iringa mkoani

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MRADI WA UUNGANISHWAJI WA UMEME WA GRIDI YA TAIFA KWA MIKOA WA LINDI NA MTWARA

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa mradi wa uunganishwaji umeme wa Gridi ya Taifa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika Mkoani Lindi leo Mei 21,

HABARI: Taasisi ya Mo Dewji yatoa msaada kwa watoto wenye saratani



Taasisi ya Mo Dewji imetoa msaada kwa watoto wanaopatiwa matibabu ya magonjwa ya saratani katika kituo cha Tumaini la Maisha katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam.

Msaada ambao umetolewa ni unga wa ngano, khanga na sabuni za kuogea, kufua na kunawia

BALOZI WA CHINA ATETA NA DK MENGI, AAHIDI KUSAIDIA MABADILIKO

 Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. Wang Ke (kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi kuhusu ushirikiano wa kibiashara baina ya makampuni ya China na Tanzania ofisini kwa mwenyekiti huyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. Wang Ke (kushoto) wakati wa mazungumzo kuhusu ushirikiano wa kibiashara baina ya makampuni ya China na Tanzania ofisini kwa mwenyekiti huyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. Wang Ke akisoma muonekano wa mbele wa kitabu kinachozungumzia maisha ya Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi ulioandikwa “I Can, I Must, I Will - The Spirit of Success” wakati wa mazungumzo yao kuhusu