Alicia Keys
Pamoja na kutajwa wasanii wengi wa nje waliofanya vizuri 2007 kama Kanye West, 50 Cent, Lil Wayne, T-Pain, Akon na wengine, jina la Alicia Keys ndiyo lilipendekezwa na wasomaji wengi wa Showbiz kuwa ndiye mwanamuziki wa nje aliyefanya vizuri zaidi kwa mwaka huu.
Ni ukweli ulio wazi kwamba, kupitia kazi yake, No One, binti huyo bado anashikilia chati za juu Bongo kwa takribani miezi kadhaa sasa kitu ambacho kinamfanya afunge mwaka kwa mafanikio.
Jahazi
Likiwa linaongozwa na Mzee Yusuph, kundi la muziki wa taarabu Jahazi ndiyo limetajwa na wasomaji wa Showbiz kuwa bora 2007. Kwa wale wapenzi wa miondoko hiyo watakuwa wamekubaliana na wasomaji wengi kwamba Jahazi mwaka huu ulikuwa wao kutokana na mafanikio waliyoyapata kwa kipindi kifupi.
Z-Anto
Msanii chipukizi aliyetajwa kufunga mwaka kwa mafanikio makubwa, hasa baada ya kuachia albamu yake yenye jina la Binti Kiziwi, huku nyimbo zake kama Mpenzi jini na huo uliobeba jina la albamu zikifunika ile mbaya.
TMK Family
Pamoja na kukumbwa na dhoruba kali, ambalo liliwafanya wagawanyike, vijana wa TMK Wanaume Family walisimama imara katika game na hatimaye watajwa kuwa kundi lililofanya vizuri mwaka huu. Pini zao kama Kazi ipo, Pisha njia, Dar Mpaka Moro, huku wakiingiza sokoni albamu tatu kwa mpigo ni ushahidi tosh
A.Y
Ndiye staa wa Bongo Flava kupitia kategori ya kizazi kipya aliyetajwa kufanya vizuri 2007. Pini lake, Usijarbu liliweza kumsimamisha katika chati mbalimbali kwa muda mrefu, huku akijiongezea miradi binafsi kama Documentary inayoelezea undani wa maisha yake na Website ambayo inamtambulisha karibu ulimwengu mzima.
Akudo
Ndiyo bendi iliyotajwa kufanya vizuri 2007. Uwezo wao mkubwa kuimba na kushambulia jukwaa ni vigezo tosha vya kuwafanya jamaa wawavutie mashabiki wengi, huku staili wanayotumia, Pekecha Pekecha ikibamba kwa sana.

No comments:
Post a Comment