Monday, December 24, 2007

WIKIENDA SHOWBIZ!

Sugu awe mshauri kwa wengine
wiki iliyopita ndani ya ‘Vice Verser’, tuliibuka na mkongwe wa Hip Pop nchini, Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu (pichani juu), tukihitaji wamshauri mambo mbalimbali kuhusiana na game ya muziki. Wasomaji kibao walishuka na ushauri wa nguvu kwa Sugu, wakiwemo hawa wafuatao.

Moja kwa moja namshauri Sugu aendelee na muziki mbona anatubamba vilivyo, asikate tamaa, asiwasikilize watu wasiojua maana ya muziki.
Yakobo D. Mwengwa, Mbagala, Dar es Salaam. 0762846900.

Namshauri Sugu abakie Ulaya atafute kitu kingine cha kufanya kuliko kunga’ang’nia muziki. Alikuwa mkali zamani kwasababu hakukuwa na wasanii wengi kwenye game, msanii aliyeimba chochote wakati ule alipata umaarufu. Alifanya vizuri alipokimbia game mara ya kwanza, lakini akakosea kurudi tena. Sio vibaya akifanya kazi ya uprodyuza na kuibua vipaji vya wasanii wachanga. 0754545478.
Huyu Sugu awe mshauri kwa wengine kwani yeye ni msanii makini na mfano wa kuingwa. 0713304297.

Ninamkubali sana Sugu kwani ni mkali wa mistari. Atulie tu mtu wetu kwani ‘gemu’ lake lipo juu. Apunguze dharau, akaze buti. James Senyegalo, Mpwapwa, Dodoma. 0717771822.

Eebwana, mimi naona Sugu astaafu tu muziki ili aweze kuitunza heshima yake kama mwanzilishi wa muziki wa kizazi kipya. Abdulmaliki Haruna, UDSM. 0714476272.

Mimi namshauri aendelee na muziki ila awe mbunifu, si anaona vijana wanavyokuja kwa kasi. Isumba Ibobo, Tanga. 0787258546.

Sugu atulie aache kutishika na chipukizi wanaokuja kila siku, kwa ufundi alionao bado yupo juu. Fara wa Bugarika, Mwaza. 0732104277.

Kwa upande wangu namshauri Sugu afungue studio vijana wanaochipukia wakarekodi kwake. Adrew M.M wa Geita. 0713980927.

Mimi namshauri aendelee na staili yake ya zamani, maana ndiyo iliyomtoa akawa juu. 0733299786.

Namshauri akaze buti kwasababu game ni tafu sana, sio kama zamani. 0755667540.


Akudo kurudi TMK
Baada ya kuacha historia katika shoo yao ya kwanza, bendi ya muziki wa dansi, Akudo Impact itarudi tena katika ukumbi wa Luxury Pub uliopo Temeke, Dar es Salaam, yakiwa ni maombi ya mashabiki wa huko.

Ndani ya safu hii, Mkurugenzi wa Mnally Promotion ambao ndiyo waandaaji, Issa Mnally alisema kwamba vijana hao wa ‘masauti’ watarudi katika ukumbi huo, Januari 10, 2008, huku wakiwa na wanenguaji wapya ambao watatambulishwa siku hiyo pamoja na nyimbo mbili mpya.

“Siku hiyo zawadi kibao zitatolewa kwa mashabiki watakao0000mudu kucheza stairi maarufu ya bendi hiyo, Pekecha Pekecha. Akudo imepania kuuanza mwaka mpya na wakazi wa TMK. Ili waweze kuwasha moto wa nguvu siku hiyo, hivi karibuni wanatarajia kuingia kambini kwa ajili ya kujifua zaidi”, alisema Mnally.

Wakazi wa Temeke watapata kulishuhudia onesho hilo ambalo limedhaminiwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti pendwa ya Uwazi, Ijumaa, Risasi, Amani, Championi na hili la Ijumaaa Wikienda kwa kiingilio cha shilingi elfu nne tu.

No comments: