Kimobiteli: Talaka kitu gani?Mwanamuziki wa bendi ya African Stars Entertainment 'Twanga Chipolopolo' Khadija Mnonga 'Kimobiteli' ameelezea kuwa hababaishwi na talaka za kila mara anazolimwa na mumewe anayefahamika kwa jina la Omary, Christopher Lissa na Richard Bukos wamefanya kazi hii.
Katika mahojiano na gazeti hili yaliyofanyika katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni Jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Kimobiteli alisema kuwa ameizoea tabia ya mumewe ya kumuandikia talaka kila kukicha na kisha kurudiana tena.
"Talaka mbona siyo 'ishu' kabisa kwangu. Yaani nimezizoea. Tokea tumeoana hii ni talaka ya nne na sijui mpaka uzeeni atakuwa ameniandikia talaka ngapi?" alieleza Kimobiteli ambaye hivi karibuni alilimwa talaka mumewe huyo.
Alisema kuwa hata hivyo muda mfupi baada ya mumewe kumlima talaka hiyo alimfuata tena kuomba warudiane.
"Kama kawaida yake akisha nipa talaka tu utaona huyo jioni anakuja nyumbani kwetu kunifuata kuomba turudiane, lakini mara hii siwezi kumkubalia tena wacha nipumzike" alieleza msanii huyo.
Aliongeza kuwa kwa sasa hana muda kabisa wa kufikiria juu ya uhusiano wake na mumewe kwani anamuuguza mama yake mzazi Bi. Dharau Mavumba.
"Hisia zangu zote hivi sasa zipo katika kumuuguza mama yangu ambaye amelazwa katika Hospitali ya Dokta Mvungi Kinondoni, siwazii masuala ya talaka kabisa. Nahitaji kutuliza akili na sina nia ya kurudiana na Omari kwa sasa" alieleza msanii huyo.

Zay B: "Sijui maumivu ya kufumania kwasababu bado sijaolewa"
Hot Corner leo imembamba Zainabu Lipangile, wengi wanamfahamu kama Zay B, ambaye yupo katika mradi wa muziki wa kizazi kipya tangu mwanzoni mwa 2000 alipochomoka na kazi iliyokuwa na jina la 'Gado', huku akijiita 'Gaidi'.
Akiwa tayari amekamilisha albamu yake ya pili, Zay B alikutana na maswali saba ya moto ambayo aliyajibu kama hivi.
1. Kati ya wazazi wako wawili, yaani dingi na maza, nani alikuwa anakupenda zaidi?
"Wazazi wangu wote walikuwa wananipenda, lakini mama alinipenda zaidi, siyo mimi tu, hata kaka na dada zangu. Mama yetu alitupenda wote, hakubagua, siunajua siku zote mama na mwana kama kuku na kifaranga"
2. Tabia gani ambazo ulikuwa nazo utotoni ambazo wazazi walikuwa hawazipendi?
"Mimi binafsi sikumbuki nilikuwa na tabia gani mbaya, lakini kaka zangu waliniambia nilikuwa mpole sana".
3. Unajisikiaje unaposikia nchi jirani kama Kenya, watu wanauana?
"Unajua siku zote mimi huwa napenda amani, haya machafuko ya Kenya yananitia uchungu sana, ukizingatia kwamba ni Waafrika wenzetu. Wanavyouana roho inauma sana, huwa sipendi hata kuziangalia picha za watu waliokufa kwenye machafuko hayo, wanawake na watoto wanakufa bila hatia. Ila nashauri nchi nyingine zijifunze kutoka kwa Wakenya kwasababu wanapigania haki yao".
4. Maradhi gani unayaogopa zaidi kuliko mengine?
"Naoga sana Ebola, Uti wa mgogo, rift valey, Kimeta na Saratani".
5. Ukiwa kama mwana jamii, unafikiri adhabu gani iwe inatolewa kwa mtu ambaye atafumaniwa na mke au mume wa mtu?
"Mke au mume wa mtu akifumaniwa ni jambo la aibu sana, pia linavunja heshima. Lakini pamoja na hayo mimi binafsi siwezi sema wapewe adhabu gani wakati wenyewe wamekubaliana wakati wakijua ni mume au mke wa mtu, isitoshe mimi bado sijaolewa, hivyo sina utaalamu wa kujua uchungu wa mume wala sijui maumivu ya kufumania. Swali hili lingewafaa zaidi waliooa au kuolewa".
No comments:
Post a Comment