Friday, July 18, 2008

IJUMAA SHOWBIZ!

Survival Sisters wako tayari kwa utambulisho

Walipokuwa wanaingia kwenye ‘game’ walikuwa wanajiita ‘Choka Mbaya Sisters’, wakafanikiwa kutoka na albamu yao ya kwanza iliyokuwa na jina la ‘Yatima’, lakini kunako mauzo wakala za uso na kuambulia jina kidogo tu, Mariam Mndeme anashuka nayo zaidi.

Sasa wanajiita ‘Survival Sisters’, huku mkononi wakiwa na albamu ya pili waliyoipa jina la ‘Tukiwezeshwa Tunaweza’. Nawazungumzia mabinti watatu, Irene Malekela, Lucy Samsoni na Latifah Abdallah wanaoonekana pichani ambao wamesema na ShowBiz kwamba, sasa wako tayari kwa utambulisho wa albamu hiyo utakaofanyika Agosti 26, ndani ya ukumbi wa Dar West Park, uliyopo Tabata, Dar es Salaam.

Zaidi wasanii hao wenye ulemavu wa viuongo ambao hivi sasa wanafanya vyema kupitia ngoma yao yenye jina la ‘Siyo siri’, iliyomshirikisha Dully Sykes, walisema kwamba mastaa kibao wa Bongo Flava wamejitolea kuwapiga tafu siku hiyo, wakiwemo Profesa Jay, Fid Q, Dully na Mr. Blu na wengine kibao.

”Siyo wasanii hao tu, pia makampuni na watu binafsi wamejitolea kutusaidia kama Global Publishers, Morgan Sound, Dotnata Decorations, Screen Masters na Times FM.

*****************************

MwanaFA: Bado nipo nipo sana

ShowBiz leo imezoza na mkali wa mashairi katika medani ya muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, ambaye kwa sasa anafoka, anatamba na kutanua katika anga za ‘FM’ na singo yake ya ‘Nipo Nipo’ ambayo imekuwa gumzo miongoni mwa vijana, hasa wale ambao nao hawajawa tayari kuoa, waki ‘bado wapo wapo tu’!.

Kwa mujibu ya mchizi, ambaye alizaliwa kwa jina la Hamis Mwinjuma, huo ni ujio wake binafsi na mpya baada ya kukamilisha ‘projekti’ aliyoifanya kwa ushirikiano mzuri na Ambwene Yesaya ‘A.Y’ ambayo ilikuwa albamu yenye jina la ‘Habari ndiyo hiyo’ iliyopokuwa na ngoma kibao zikiwemo ‘Asubuhi’ na ‘Ngoja ageuke’. Amewataka mashabiki kukaa tayari kwa vitu vikali zaidi kutoka katika project yake mpya.

**************************

King of Hip Hop

Kala atupwa nje!

Haya sasa! Mambo yameanza kupendeza ndani ya shindano la kumtafuta mkali wa michano ya Ki-Hip Hop (King Of Hop Hop) linaloendeshwa na gazeti hili. Nachotaka kukwambia ni kwamba tayari washiriki wameanza kutupwa nje, yaani yule anayepata kura chache zinazopigwa na wasomaji na mashabiki wa wasanii waliotajwa kuwemo shindanoni.

Mabibi na mabwana, kwa mujibu wa kura za mashabiki na idhini kutoka kwa mratibu wa shindano hilo, Charles Mateso, ShowBiz inachukua fursa hii kumtaja msanii Kala Jeremiah kuwa ndiye aliyefungua pazia la kutoka baada ya kupata kura chache kuliko washiriki wengine tisa wanaowania taji hilo.

”Kala, ambaye ni mmoja wa wasanii wakali nchini alipigiwa kura na mashabiki wengi lakini pamoja na hayo bado kura zake zilionekana chache hivyo kujikuta akiondolewa katika kinyang’anyiro hicho. Kwa kifupi shindano ni gumu, wasanii wanaonekana kuchuana vikali kwa kupishana kwa kura chache, kitu kinachotufanya tushindwe kutabiri nani ataibuka na ushindi huo” alisema Mateso.

Aidha mratibu huyo alisema kwamba, ni wakati wa Watanzania kumpigia kura msanii wanayempenda ili kumuwezesha kunyakua taji hilo litakalomjengea heshima na historia katika maisha yake ya kimuziki na kuwataja washiriki waliobaki kuwa ni Profesa Jay, Black Rhino, Chid Benz, Fid Q, Langa, Kalapina, Rado na Lord Eyez wa Nako2Nako.

”Nawaomba mashabiki wa muziki wa Hip Hop waendelea kupiga kura wakimtaja msanii ambaye wanahisi uwezo wake upo juu ili awe mshindi kwa kuandika neno HP (acha nafasi), kisha jina la msanii, halafu watume kwenda namba 15551. Kumbuka hata wewe msomaji utajishindia zawadi kibao kwa kutuma sms nyingi zaidi”, alisema Mateso.

*************************

No comments: