Saturday, July 26, 2008

IJUMAA SHOWBIZ!

Bahati Bukuku kuwakutanisha mastaa wa Injili

Msanii wa nyimbo za injili nchini Bahati Bukuku anatarajia kuwakutanisha baadhi ya mastaa wa fani hiyo kwenye utambulisho wa albamu yake ya tatu, ‘Nisamehe Siyo Majaribu’ utakaofanyika ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee Julai 27, mwaka huu.
Ndani ya ShowBiz, msanii huyo alisema kwamba, baadhi ya wasanii wakubwa wa Nyimbo za Injili kama Rose Mhando, Jennifer Mgendi, Bonifasi Mwaitege, Mwansasu na Ancy Mwalukasa watakuwepo kwa ajili ya kumsaidia kuhubiri neno la Mungu siku hiyo.

King of Hip Hop:
Black Rhino amfuata Kala Jeremiah

Lile swali la nani kumfuata kala Jeremiah katika shindano la kumtafuta Ijumaa King Of Hip Hop linajibiwa leo. Kwa mujibu wa wasomaji na mashabiki wa Sanaa ya Hip Hop nchini, msanii Nicholas Haule ’Black Rhino’ ndiyo ameuaga mpambano wiki hii.
Rhino ambaye hivi sasa anakimbiza na ngoma zake mbili, ‘Vaa tutoke’ na ‘Black Chata’ zilizopo kunako albamu yake ya kwanza ambayo tayari ipo kitaani, ameondolewa shindanoni baada ya kupata kura chache zaidi tofauti na wasanii wengine waliobaki katika mpambano huo.

Kwa mujibu wa mratibu wa shughuli hiyo Charles Mateso, hivi sasa shindano la Ijumaa King Of Hip Hop limebaki na washiriki nane ambao ni Fid Q, Chid Benz, Kalapina, Profesa Jay, Langa, Rado, Johmakini na Lord Eyes.

“Tunawaomba wasomaji na wapenzi wa Sanaa ya Muziki wa Hip Hop waendelee kupiga kura zao wakimtaja mshiriki ambaye wanadhani anastahili kuwa mshindi kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) na kuandika neno HP kisha wanaacha nafasi, wanataja jina la mshiriki kisha watume kwenda namba 15551. Zawadi kwa wasomaji watakaotuma kura nyingi zinaandaliwa,” alisema Mateso.
*****************

1 comment:

Anonymous said...

Mbona waimbaji wa gospel such as Upendo Kilahilo hawakaribishwagi, au mnamuonea vivu nini?