Wednesday, July 23, 2008

MASIKINI TID!


Medani ya muziki wa kizazi kipya imepigwa butwaa leo baada ya mwanamuziki TID, kwa mara ya mwisho akitamba na wimbo wake Nilikataa, kuhukumiwa kwenda jela kutumikia mwaka mmoja kwa kosa la kumpiga mtu hadharani na kumsababishia maumivu ya mwili, mwaka jana, pale Slipway Hotel. Hii imekuja kama kumkomoa msanii huyo kutokana na 'kahistoria kake' ka nyuma ka ishu za 'polisi polisi' kila mara. Kwani kabla ya kukumbwa na kesi hii, aliwahi kukabiliwa na kesi ya ubakaji na kufikishwa mahakamani kabla ya kunusurika kimiujiza na kifungo..... mara nyingi kwa kosa kama lake, adhabu huwa ni faini na huenda Khaleed Mohamed hakutarajia kwenda jela...dah!!!

6 comments:

Anonymous said...

JELA NI YA KILA M2 WA2 WANGU LEO T.I.D KESHO MIMI KESHOKUTWA WEWE NANI ALITEGEMEA JAMAA ATKULA NYUNDO 1...I HATE HUYO JAMAA ALIEMPAKAZIA KESI.HE FUCKED UP TO TID.

Anonymous said...

JELA NI YA KILA M2 WA2 WANGU LEO T.I.D KESHO MIMI KESHOKUTWA WEWE NANI ALITEGEMEA JAMAA ATKULA NYUNDO 1...I HATE HUYO JAMAA ALIEMPAKAZIA KESI.

Anonymous said...

What goes around comes around, kama jamaa alimpakazia asubiri na yeye.........!

Anonymous said...

kuwa na uhakika wewe ulieandika hio msg hapo juu Jamaa kweli kampiga mtu na mimi nilikuwepo that day Slipway + TID mwenyewe kakubali mahakamani sasa inakuwaje wewe unasema amempakazia.....KUWA NA FACTS

Anonymous said...

Acheni kubabaika kama kweli kampiga anastahili adhabu ila adhabu alopewa ni kubwa kulingana na kosa hilo ndio suala lakini unasemaje kampakazia kama yeye mwenyewe kakubali Bwasheikh? au ndio kubababaika kwakuwa ni TID sio?

Bado ananafasi ya kukata rufaa

Anonymous said...

Iwe fundisho, sio kwa kuwa ni maarufu uwe unapiga watu kwa kuwa tu umelewa, Acheni hizo wachangiaji msio na uhakika wa kilichotokea