Monday, July 28, 2008

Mastaa hawa walivyoipokea hukumu ya TID

Kalapina:
Kwa upande wangu mimi nilishangaa TID kuhukumiwa kifungo, kwasababu siku ya tukio tulikuwa wote ukumbini, huyo dogo aliyemshitaki ndiye alikuwa na matatizo. Wiki hii tunakata rufaa, naamini siku chache zijazo TID atakuwa nje
AY:
Ilinishutua sana, nimesikitika sana. Sikutegemea habari kama hiyo kwa kipindi hiki

Stara Thomas:
Du! Kwa kweli nilisikitika sana ila hakuna jinsi, kama kweli alipatikana na hatia atulie tu, hata familia yake pia itulie. Ni jambo linaloweza kumpata mtu yeyote, watulie tu mwaka utaisha atatoka, Mungu yupo. Ila sasa ni muda wa wasanii wote kuwa waangalifu sana na vitu tunavyofanya, maisha hayatabiriki
Dudu:
Binafsi ilinishtua, ukizingatia kwamba nilikuwa sijui kama TID alikuwa na kesi. Ila nahisi TID alifanya uzembe kwa kudharau, kwasababu kesi kama hizi watu huwa wanamalizana kwa kuombana msamaha tu. Nasikitika kwasababu amefungwa kipindi hiki ambacho wasanii huwa tunatengeneza pesa sana, pia bendi yake, Top Band itakuwa katika wakati mgumu sana

Prof J:
Ilinishtua sana, yaani kama naota, imeniuma lakini pia imenifundisha kuwasamehe wale wote niliokuwa na bifu nao. Nampa pole sana TID, kwasababu wote tuko chini ya sheria na tunaiheshimu.
Fid Q:
Niliipokea taarifa hiyo kwa masikitiko, lakini haijanishtua sana kwasababu nilitegemea kitu kama hicho. Kuna baadhi ya watu wana chuki na sisi wasanii, cha msingi ni kuwa makini ndiyo kitu nilichojifunza

Madee:
Binafsi nahisi kama ni promosheni ambayo TID alikuwa anaitaka. Mtu kama yeye siyo wa kukosa laki mbili. Nauhakika mpaka wiki hii iishe TID atakuwa nje

TOP IN JAIL!

2 comments:

Anonymous said...

Katika maoni yote hapa utaona jinsi shule au upeo wa mawazo/busara ulivyokomaa kwa hao wasanii!!!.Stara nambari one, wengine wa - grade

Lulu Komanya said...

umefika wakati kwa wasanii wajifunze kutokana makosa, na pia wajue kuwa usanii sio kitu kidogo kutokana na wao watu wanajifunza mengi, sasa kama watakuwa na tabia ambazo haziridhishi je jamii itajifunza nini kutoka kwao?? pia tuache mambo ya kuiga mila na desturi za watu wengine inabidi tusimame kama watanzania halisi na si vinginevyo.