Monday, September 29, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ

Matumaini:sitoki faragha na Kiwewe
Kutoka ndani ya Kundi la Sanaa za Maigizo, Kaole, ‘Hot Corner’ ilipata kupiga stori na mkali wa ‘komedi’, Tumaini Mwakibibi a.k.a Matumaini ambaye aliongea ishu kibao ambazo wewe msomaji utazinyaka kutoka hapa, zaidi tucheki na Rebeka Bernard kwa ‘intavyuu’ zaidi.

Hot Corner: Mambo vipi Matumaini?
Matumaini: Yapo fresh tu.
Hot Corner: Unajisikiaje kuwa staa wa Bongo?
Matumaini: Najisikia vizuri kwasababu ndiyo ilikuwa ndoto yangu haswa.
Hot Corner: Unadhani utakuwa hujakamiliki bila kuwa na nini?
Matumaini: Bila sanaa ya maigizo.
Hot Corner: Kuna tetesi kuwa unatoka faragha na masanii mwenzako, Kiwewe, hiyo ikoje?
Matumaini: Hakuna kitu kama hicho, yule ni msanii mwenzangu.
Hot Corner: Starehe yako kubwa ni ipi?
Matumaini: Kucheki muvi.
Hot Corner: Msanii gani Bongo anayekuvutia?
Matumaini: Marlaw ananikosha sana.
Hot Corner: Kipi kinachokukera nje ya sanaa?
Matumaini: Watu wazima wanaofanya mambo ya kitoto.
Hot Corner: Msanii gani alikuvutia ukaingia kwenye sanaa?
Matumaini: Kemmy.
Hot Corner: Unapenda mume wa aina gani ?
Matumaini: Atakayekubaliana na matakwa yangu.
Hot Corner: Poa, aksante sana kwa ushirikiano wako.
Matumaini: Nawe pia, karibu tena.
***************************************
Cellulant yagawa shavu kwa wasanii wa Bongo
Kampuni mpya ya milio ya simu Bongo, Cellulant imezindua rasmi mradi wa kununua nyimbo za wasanii na kuziuza kisha wasanii hao kufaidika kwa kiasi cha mkwanja kitakachopatikana, ishu ambayo tunaweza kusema ni shavu au dili kwa wasanii hao, cheki na Richard Bukos.

Akisema na safu hii katika uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Hoteli ya Southern Sun, Dar es Salaam, Afisa Mwandamizi wa kampuni hiyo, Jide Harrison alitamka kwamba katika mpango huo kampuni yake itachukua nyimbo za wasanii na kuziuza kwa watumiaji wa simu za mkononi kwa shilingi 600.

“Katika kiasi hicho, msanii atapata shilingi mia moja kila wimbo wake utakaponunuliwa pesa ambayo atakuja kuchukua kwenye kampuni yetu kila mwezi tofauti na walanguzi ambao wanahamisha kienyeji nyimbo za wasanii na kunufaika wao peke yao,” alifafanua Jide.
************************************

TMK Family:..wajidhamini wenyewe
Tofauti na ilivyozoeleka na watu wengi kwamba, wasanii huwa hawana uwezo wa kujiandalia shoo wenyewe zaidi ya kualikwa na mapromota, usemi ambao kundi la TMK Wanaume Family limeufuta kwa kujiandalia shoo lenyewe, huku wakijidhamini kupitia maduka yao ya nguo, la Mbagala na lile la Temeke, Dar es Salaam, cheki na Issa Mnally.

Meneja wa kundi hilo, Said Fella alisema na safu hii kwamba, shoo ya kwanza itagongwa siku ya Idd ndani ya Ukumbi wa Basiaya Camp uliopo Boko, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, huku ya pili ikifanyika siku ya Idd pili kunako ukumbi wa Dar West Park Tabata.

“Katika shoo hizo maalum kwa ajili ya kusherehekea sikukuu hiyo, tutatambulisha kazi kibao ukiwemo wimbo mpya wa Mh. Temba ambao unaoitwa ‘Kiulaini,” alisema Fella.
******************************


Sostenes alipokuwa Hon Kong!
Picha mbili za juu ni Bw. Sostenes Raphael akiwa Hon Kong mapema wiki iliyopita alikokwenda baada ya kushinda Bahati Nasibu ya Jishindie Safari ya Hon Kong 2008 iliyokuwa ikiendeshwa na gazeti la Ijumaa Wikienda. Sosteness amerejea Dar jana saa nane mchana.

No comments: