Saturday, December 27, 2008

MANDHARI YA HARUSI DAR

Huu ni ukumbi wa Twiga uliyopo Mbezi, ambako kuna kumbi mbili zilizojengwa maalum kwa shughuli za harusi na ni miongoni mwa hall zilizo 'full air conditioned'. Picha hii ilipigwa muda mfupi kabla ya wageni waalikwa na maharusi kuingia ukumbini.
Mara nyingi hivi ndivyo inavyopambwa sehemu wanayokaa maharusi...hapa palikuwa pamepambwa maalum kwa bibi harusi mtarajiwa wakati wa Send Off party yake.
Huu ni ukumbi wa Banora unavyoonekana kwa nje ukiwa tayari kwa shughuli ya harusi..ni miongoni mwa kumbi maarufu jijini Dar kwa shughuli hizo
Harusi nyingi hutumia mtindo wa 'self service' linapokuja suala la chakula na huwa kuna mchanganyiko wa vyakula mbalimbali kama wali, ndizi, nyama, chapati, n.k

Usafiri wa harusi nyingi jijini Dar huwa ni gari aina ya Mercedes Benz, wachache hutumia aina nyingine za magari kama BMW, Limousine au Toyota.
(MANDHARI YA HARUSI DAR ni safu mpya itakayowaletea picha kutoka harusini mara kwa mara...nawe pia kama utakuwa na picha maalum kwa ajili ya ku share na wasomaji wengine unaweza kunitumia: abbymrisho@gmail.com)

No comments: