Monday, July 27, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!


Amelle Berrabah.
Kanye West; afukuzia toto la Sugababes
Inaelezwa kuwa hivi sasa Kanye anamfukuzia mrembo anayefanya muziki kwenye Kundi la Sugababes la Uingereza, Amelle Berrabah.

Ishu imewekwa mtandaoni kwamba Kanye ambaye hivi karibuni alitemana na aliyekuwa mpenzi wake, Amber Rose ingawa walionekana wakiwa pamoja hivi karibuni kwenye Tuzo za BET, atafanya makeke kuhusu Amelle akiwa UK.

Sosi wa habari alisema: “Kanye anatarajia kwamba kila kitu kitakuwa sawa akiwa UK.
“Kanye alikuwa na Amelle alimsaidia pamoja na wanamuziki wengine wa Sugababes hivi karibuni. Amepanga kukutana naye kwa ajili ya masuala ya muziki.

“Hata hivyo, Amelle amekuwa akimchukulia Kanye kama kaka yake mkubwa, ingawa Kanye mwenyewe amesema kuwa mambo yatakuwa tofauti ikiwa Amelle mwenyewe akitaka.

Haionekani kama Kanye atakaa na kumsubiri Amelle ambaye alikutana naye kwa mara ya kwanza kwenye Tuzo za MTV Europe Music miaka miwili iliyopita.

Hata hivyo, wakati ikielezwa hivyo, mtandao unaodili na ishuz za uhusiano wa mastaa unaeleza kwamba Amelle amewahi kujikunja kimahaba na Kanye kati ya mwaka 2007 na 2008. katika mtandao huo, inaelezwa kwamba rapa huyo alianza kujiachia na Alexis Eggleston kuanzia mwaka 2002 kabla ya mwaka 2005 kuhamia kwa mwanadada Brooke Crittention na mwaka 2007 Amelle Berrabah,

Pia Kanye amewahi pia kujiachia na Amber Rose mwaka 2008 pamoja na Jennifer Metacarlfe kabla ya kuhamisha majeshi yake ya Rihanna.

Hivyo, kwa jumla Kanye amekwishajikunja na totoz sita, hiyo ni kwa mujibu wa mtandao huo unaodili ishuz za malavidavi kwa mastaa.

Listi hii tumewahi kuitoa huko nyuma lakini leo tume-flash back ili kuona ni kwa namna gani staa huyo wa Jesus Walk alivyo fundi katika sekta ya vimwana. Ebwana Dah! Jamaa hakamatiki.
******

Ujio mpya wa Jigga Rihanna naye ndani
Stadi wa R&B, Robyn Rihanna Fenty, Bendi ya MGMT ni miongoni mwa wasanii watakaoshirikishwa katika albamu mpya ya Rapa Sean Cutter ‘Jay-Z’, imefahamika.

Nyeti za mtandaoni zinaeleza kuwa pamoja na Rihanna, wasanii wengine watakaoshiriki katika ujio wa albamu mpya ya mkongwe huyo ni underground Drake, Kud Cudi na Mr. Hudson.

“The Blueprint 3 ni albamu inayoonesha ukomavu wangu katika gemu,” alisema Jay-Z a.k.a Jigga ambaye ana mpango wa kustaafu muziki hivi karibuni.

“Ukiwa rapa mwenye zaidi ya miaka 30 na bado ukawa unafanya mambo kama kijana mwenye umri wa miaka 15 ni jambo la kujivunia,”aliuambia mtandao wa Reuters.

Alisema kuwa wasanii ambao wanaweza kujilinganisha uwezo wao kwa hivi sasa ni Kanye West, Timbaland na Lil Wayne lakini yeye umri umeanza kumpa kisogo.
Hata hivyo, rapa anayekuja kwa kasi, Lil Wayne hatashiriki katika uzinduzi wa msanii huyo uliopangwa kufanyika Septemba 11, mwaka huu.

Jay-Z alisema kuwa ikipita miaka mitatu baada ya yeye kustaafu, mashabiki wake ipo siku watakuja kushtuka na kugundua uwezo wake kipindi hicho yeye akiwa nje ya muziki.

Wimbo mpya wa The Blueprint 3 unatarajiwa kutambulishwa rasmi kwa mashabiki Ijumaa ijayo ambapo Kanye West na Rihanna wamealikwa pia katika utambulisho wa wimbo huo.
****
Sijasimama, sijakaa, nimeheng - Bob Haisa
Mwanamuziki kiraka, Haisa Mbyula ‘Bob Haisa’ amesema kwamba hivi sasa hajaweza kusimama kimuziki lakini hajakaa kwa sababu ni matumaini yake kuwa one day mishemishe zake zitalipa.

Bob aliimegea Ijumaa Showbiz hapa juzi kati kuwa kinachosababisha mpaka sasa awe hajaidondosha kitaani albamu yake ya Ubeleko ni ubize alionao promota wake, John Dotto.

“Mtu mzima Dotto ana mishemishe nyingi ndiyo maana program za kuingiza albamu mtaani zinasuasua lakini mambo yakiwa yes utaona. Namngoja mkubwa awe fresh,” alinena Bob.
**********
Kanumba; bize kwa Malkia Elizabeth na dude jipya
Stadi wa filamu nchini, Steven Charles Kanumba yupo bize kwenye himaya ya Malkia Elizabeth II, akirekodi mauzo ya sura kwenye dude jipya litakalodondoka kitaani kwa jina la Lovely Gamble.

Kanumba a.k.a The Great yupo UK akifanya kweli kwenye muvi hiyo ambayo inarekodiwa katika miji ya Leicester, Reading, London na Birmingham nchini Uingereza.

The Great says halla 2 fans wake wa Bongo na kuongeza: “Ni filamu inayoandaliwa na maprodyuza wa UK na Bongo. Yumo Asha Baraka wa Tanzania, Frank Iyembe na Alan Kalinga wa UK. Hii itakuwa bora kuliko zote nilizowahi kuuza mtu wangu.”

Wakati Kanumba akiwa kwa Malkia, hivi sasa anasubiriwa kwa hamu Bongo ili auze sura akiwa bega kwa bega na Vincent Kigosi ‘Ray’ kwenye muvi ya Tears on Valentine Day ambayo imetungwa na mtunzi mwenye jina kubwa nchini, Eric Shigongo James.
******************************
Artists Bongo hawapo ki-professional
Its all about kuwekana kwenye mstari, hii ni kwa asilimia kubwa ya artists wa Kibongo ambao bila kuzingatia nafasi waliyonayo, wamekuwa wakiidhalilisha taaluma yao mbele ya mashabiki.

Iko hivi, artist anaweza kualikwa kwenye shoo na mkwanja akalipwa ambao anakuwa ameridhika nao, si unajua kibongo bongo? A problem comes kwenye kujisahau na kutaka aonekane mtu wa kujichanganya.

Akifika ukumbini badala ya kuyatenga kwenye sehemu inayotakiwa, anageuka mr. roving, kila kona anaonekana akijimix na fans, eti anadai anashoo love. Haiko sawa, haijatulia hii jambazi langu!

Sometimes things turn worse, artists hao wanapovuka mipaka, hapo tunamaanisha kuwa kujichanganya kwao hakuishii kwenye stori na kufanya cheers, badala yake wanagandamizia na mizinga kabisa. Wanaomba mkwanja!

Hii si kwa wana Bongo Flava peke yao, kwenye dansi hili ni tatizo sugu. Msanii anarandaranda kwenye kona za mashabiki na kupiga mizinga ya hapa na pale, anaomba kununuliwa bia. That’s a shame men!

Kimsingi wanachokifanya ni kutokujua thamani yao, wanaji-embarrass wenyewe, matokeo yake wanaanza kuonekana ni wa kawaida na kwenye shoo zao attendance inapungua. Heshima kwanza wewe musician.

Kitendo hiki cha kupiga mizinga bila mpango inaonekana wazi kuwa wasanii wetu hawajui taaluma yao. Yap, hawapo ki-professional! That’s why wanachuja within kitambo kifupi!
****
compiled by mc george

No comments: