Friday, August 21, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

IJUMAA SEXIEST BACHELOR: Jerry Tegete, Makamua ndani ya mpambano, kura wiki ijayo
The Soccer Bongo, Jerry Tegete na vocalist wa kiwango cha juu katika eneo la muziki wa R&B nchini, Makamua a.k.a Mwana wa Sekimanga wamepigiwa kura ya kuingia katika Top 12 ya Ijumaa Sexiest Bachelor 2009.

Kama unainyaka uzuri ni kwamba wiki iliyopita, tulitoa majina ya wakali wanne, ukitakiwa kupiga kura ili kuchagua watu wawili ambao wanatosha kuingia katika Top 12 kabla ya kuchapa mwendo kuelekea kumpata mshindi wa taji.

Orodha ni hiyo, wiki ijayo tutatoa taratibu maalumu ya wewe kushiriki kunako mpambano huu kwa kupiga kura. Tuko sawa.

***********************************************



KWA SATILI HII, KANUMBA KAFUNIKA!
Wengi wamezoea kumuona Kanumba akiigiza kwa kutumia magari na nyumba za kifahari maeneo ya mijini, lakini safari hii amekuja tofauti baada ya kuigiza filamu yake ya Village Pastor akiwa katika maisha duni ya kijijini.

Wakiongea na ShowBiz, wadau wa filamu Bongo, ambao wameona picha alizopiga Kanumba akiwa anaendesha baiskeli na akiwa amaevaa nguo za kizamani kijijini, walisema kuwa filamu hii itafunika zingine alizowahi kucheza kijana huyu ambaye kwa sasa anatamba na muvi yake mpya ya The Director ambayo amewashirikisha wasanii kibao maarufu kutoka Nigeria.

Village Pastor amecheza na mwanadada Aunt Ezekiel ambaye naye ameigiza kama mpenzi wa Kanumba kijijini na kufunika vilivyo.....kaa mkao wa kula kuiona filamu hii inayotarajiwa kuingia mtaani hivi karibuni.
**********************************************






Tears on Valentine’s Day: Ni Next Level!
Muvi ambayo inaendelea kurekodiwa hivi sasa, Tears on Valentine’s Day (kama pichani juu) itakuja na vitu tofauti ambavyo waandaaji wengi wa Bongo huvikwepa wakati wa kuandaa filamu zao kutokana na kukwepa gharama.

“Tunataka kuonesha kuwa Tanzania tunaweza kuwa mbele zaidi, muhimu ni kujipanga. Wasanii tuliowachukua kwa ajili ya kurekodi ni wa kiwango cha juu sana (Next Level), mandhari inayotosheleza mahitaji ya stori ya filamu na picha za kiwango cha juu,” alisema Hamie ambaye ndiye muongozaji wa muvi hiyo.

**********************************************

Kingwendu alizwa M na nusu
Komedian aliyekwenda eji Bongo, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’ ameingizwa mjini na promota mmoja jijini Mwanza.

Kingwendu spoke to Showbiz mapema wiki hii kwamba, promota huyo amemtia ndani kiasi cha fedha shilingi milioni 1.5 ambazo aliziingiza baada ya kupiga mzigo Kanda ya Ziwa.

Said: “ … (anataja jina la mtu aliyemliza) amenifanyia kitu kibaya sana, alinichukua vizuri Bongo akanipa advance, kula, kulala haikuwa na matatizo, kwahiyo nikamuamini lakini kumbe siyo mtu kihivyo.

“Baada ya kupiga shoo kwenye vijiji vya Zalagula, Kasaratu, Nyanango na Kanyala jijini Mwanza, nilikuwa nimekusanya shilingi milioni 1.5 kibindoni lakini juu kwa juu nilipata ‘dili’ kwahiyo nikaunganisha shoo.

“Promota wangu aliniomba nimpe pesa hizo ili akaniwekee kwenye akaunti yangu, mimi kwa sababu nilikuwa nimeshamuamini nilimpa lakini huwezi kuamini, baada ya hapo kila nikimpigia simu ni stori tu. Hivi sasa nimemfungulia mashataka polisi kwa kosa la wizi wa kuaminiwa.”
***********************************************
compiled by mc george

2 comments:

Anonymous said...

kumbe kingwendu we cha mtoto tu,sasa utamuaminiji mtu akuwekee pesa bank kwani wewe ulishindwa nini kwenda kuzipeleka mwenyewe eeh kingwendu mbona hivyo tena.

SEDOUF said...

hahahahahahahah!
pole sana kichaa wangu!
kutokana na furaha ninayoipata na familia yangu kupitia filamu zako .nahisi ipo haja ya kukupunguzia maumivu ya dhuluma.tuma chanzo cha mawasiliano ili nione nini naweza kufanya!
Kaka usiwaamini walimwengu kiasi hicho!
heno!heno!
(serious weka mtandao wazi tuokowe jahazi)